Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 323 2025-05-15

Name

Mwanaisha Ng'anzi Ulenge

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: -

Je, upi mkakati wa kuwaandaa Wanawake wakulima wa mbogamboga Mkoani Tanga kwenye mpango wa Tanga kuwa hub ya kilimo cha mbogamboga?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa engineer Mwanaisha Ulenge, kama ifuatavyo: -

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo imekiwezesha Kituo cha Utafiti cha Mlingano TARI kuwa kituo mahiri katika uzalishaji wa mazao ya viungo, karafuu na mboga. Pia Wizara inaendelea kutoa mafunzo ya kanuni na teknolojia bora za kilimo cha mboga kushirikiana na sekta binafsi ikiwemo TAHA kujenga vituo na miundombinu ya kuhifadhi mazao ya mbogamboga ikiwemo vyumba vya baridi na kutoa mafunzo ya ukusanyaji, ufungashaji na uhifadhi wa mazao kabla ya kusafirishwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi.