Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 1
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imekwishafanya tathmini na kubaini nyumba 84 pamoja na fedha bilioni 1.8: -
Je, ni lini ukarabati utaanza?
Mheshimiwa Spika, swali la pili; katika Halmashauri ya Shinyanga kuna kituo cha afya ambacho ni chakavu tagnu enzi za mkoloni, na pale ni Makao Makuu ya Halmashauri ya Shinyanga: -
Je, ni nini mkakati wa Serikali wa kuhakikisha kwamba inajenga kituo kipya cha kisasa?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Christina Christopher Mnzava, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama tulivyojibu jibu la msingi, tathimini ishafanyika na ukarabati utaanza huu mwaka wa fedha 2026/2027.
Mheshimiwa Spika, swali la pili, kuhusu mkakati wa kujenga kituo kipya kwenye Manispaa ya Shinyanga, nimuhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imekuwa ikijenga vituo vya polisi kupitia bajeti ya Serikali pamoja na mfuko wa tuzo na tozo. Kwa hiyo, tumechukua kituo hicho alichokitaja kwenye manispaa hiyo, tutakiingiza kwenye mpango na kutengewa fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Ahsante sana.
Name
Mwita Mwikwabe Waitara
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tarime Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 2
MHE. MWITA M. WAITARA: Mheshimiwa Spika, Zima Moto Wilaya ya Tarime, hawana gari, hawana ofisi. Kwa hiyo utendaji wao kazi ni mgumu kwelikweli na wanashusha hadhi ya jeshi hilo. Je, ni lini Serikali itatoa huduma hizo muhimu kwa watu wale wafanye kazi kwa heshima? Ahsante.
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mwita Waitara, Mbunge wa Tarime Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Zima Moto, Serikali imeshaagiza na kununua magari 150 kwa ajili ya wilaya zote hapa nchini, ikiwepo na Wilaya ya Tarime.
Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu ofisi, nitoe wito kwa Mheshimiwa Mbunge na halmashauri itenge eneo tayari kwa ajili ya kuingiza kwenye mpango na kujenga Ofisi ya Zima Moto katika Halmashauri ya Tarime. Ahsante sana.
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 3
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Mbulu ni wilaya kongwe nchini, makazi ya Askari Polisi na Magereza katika wilaya hiyo ni chakavu sana. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kujenga makazi mapya na kukarabati yale yaliyopo? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Zacharia Issaay, Mbunge wa Mbulu Mjini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kila mwaka imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa makazi ya Askari Polisi na Magereza hapa nchini. Na hiki cha mji wa Mbulu pia tutakichukua kuingiza kwenye mpango na kutengewa fedha kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Ahsante sana.
Name
Flatei Gregory Massay
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Vijijini
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 4
MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, Jimbo la Mbulu Vijijini ina vituo vitatu vya Polisi na Mheshimiwa Naibu Waziri, unavijua na hakuna makazi kabisa ya polisi. Je, lini unaweka hata bajeti ya kujenga makazi haya?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Flatei Massay, Mbunge wa Mbulu Vijijini kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, Serikali inatenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa makazi ya Askari Polisi. Kwa hivyo alivyovitaja vya Wilaya ya Mbulu Vijijini pia tutavichukua tayari kuingiza kwenye mpango na kutengewa fedha kwa ajili ya kufanyia ujenzi. Ahsante sana.
Name
Esther Nicholus Matiko
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 5
MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, makazi ya Askari wa Jeshi la Magereza nchini ni chakavu sana, hasa Gereza la Tarime na Gereza la Matongo, lililopo Mkoa wa Simiyu. Ninataka kujua mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba wanaboresha makazi haya ya Askari wa Jeshi la Magereza?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Esther Matiko, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye jibu la msingi, Serikali imekuwa ikifanya tathimini ya uchakavu wa makazi ya Askari Polisi na Magereza hapa nchini na nimuhakikishie Mheshimiwa Esther, pia na ya Tarime tutaingiza kwenye mpango na tayari kwa ajili ya kufanyiwa ukarabati. Ahsante.
Name
Minza Simon Mjika
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 6
MHE. MINZA S. MJIKA: Mheshimiwa Spika, majengo ya Askari Polisi Mkoa wa Simiyu ni hakuna kabisa tuseme hivyo, lakini Wilaya ya Maswa ni wilaya ambayo ni kongwe, haina kabisa majengo ya Askari Polisi na majengo yaliyopo yamechakaa kabisa yapo chini ya kiwango. Je ni lini Serikali itajenga makazi mapya?
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Minza Mjika, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, tutachukua nyumba za Askari Polisi ambazo hazipo kabisa kwenye Wilaya ya Maswa ili tuingize kwenye mpango na kutengewa bajeti kwenye miaka ya fedha ianyokuja. Ahsante.
Name
Maryam Azan Mwinyi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Chake Chake
Primary Question
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: - Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?
Supplementary Question 7
MHE. MARYAM AZAN MWINYI: Mheshimiwa Spika, je ni lini Serikali itazifanyia ukarabati makazi ya Polisi, nyumba zilizopo Kengeja na mkoani, mkoa wa Kusini Pemba? (Makofi)
Name
Daniel Baran Sillo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Babati Vijijini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali imekuwa ikitenga fedha kila mwaka kwa ajili ya ukarabati wa nyumba za Askari Polisi kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge, mkoani kule Pemba. Lakini nimuhakikishie pia maeneo haya aliyoyataja pia tutakaa na Mheshimiwa Mbunge, tutaingiza kwenye mpango tayari kwa ajili ya kutengewa fedha kwa ajili ya ukarabati wa makazi hayo. Ahsante. (Makofi)