Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 322 2025-05-15

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA aliuliza: -

Je, nini mpango wa Serikali wa kuboresha makazi ya Askari Polisi Manispaa ya Shinyanga kwa kuwa ni duni sana?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Serikali inatambua uchakavu wa nyumba za makazi ya askari polisi katika manispaa ya Shinyanga na mikoa yote kwa ujumla hapa nchini. Katika Manispaa ya Shinyanga zipo jumla ya nyumba 84 za makazi ya askari polisi ambazo ni chakavu. Tathmini ya uchakavu kwa ajili ya kuzifanyia ukarabati nyumba hizo imeshafanyika na kiasi cha fedha shilingi 1,848,000,000 kinahitajika.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutenga fedha toka kwenye Bajeti yake kila mwaka wa fedha ili kuweza kukarabati nyumba za makazi ya askari polisi hapa nchini zikiwemo za Manispaa ya shinyanga. Ahsante.