Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

George Natany Malima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpwapwa

Primary Question

MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: - Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kuimarisha kingo za korongo linalopita katikati ya Mji wa Mpwapwa ili kuzuia mmomonyoko na madhara kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. GEORGE N. MALIMA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa jibu zuri la Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, wananchi wa Mpwapwa wangependa kusikia: -

Je, ni lini hiyo tathmini ya kina itakamilika ili ujenzi uanze mara moja?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; ili kuweka uzito wa changamoto hii kule Mpwapwa: -

Je, Mheshimiwa Waziri yuko tayari kutembelea Mpwapwa ili kujionea mwenyewe madhara yaliyosababishwa na hilo korongo?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, jambo hili ni la dharura kwa hiyo Serikali inalifanyia kazi kwa udharura katika kuhakikisha kwamba tathmini hii inakamilika ndani ya kipindi kifupi. Ninaomba Mheshimiwa Mbunge awe na Subira wakati jambo hili linafanyiwa kazi.

Mheshimiwa Spika, kuhusiana na kutembelea eneo hilo, Serikali iko tayari, itatuma wataalamu wake ikiongozana na Waziri husika ili kuweza kwenda kujionea.