Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 25 | Union Affairs | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 321 | 2025-05-15 |
Name
George Natany Malima
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mpwapwa
Primary Question
MHE. GEORGE N. MALIMA aliuliza: -
Je, lini Serikali itaanza ujenzi wa kuimarisha kingo za korongo linalopita katikati ya Mji wa Mpwapwa ili kuzuia mmomonyoko na madhara kwa wananchi?
Name
Eng. Hamad Yussuf Masauni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kikwajuni
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII K.n.y. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kutokea kwa korongo linalopita Katikati ya Mji wa Mpwapwa kumesababishwa na athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uwepo wa mvua nyingi pamoja na shughuli zisizoendelevu za ukataji miti, kilimo na ufugaji katika safu za Milima Kiboriani. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa inaendelea kufanya tathimini ya kina ya ujenzi wa kingo za korongo linalopita katikati ya Mji wa Mpwapwa. Lengo la tathmini hiyo ni kubainisha gharama za ujenzi wa ukuta katika kingo hizo ili kupunguza mmomonyoko wa udongo na kunusuru maisha na makazi ya watu wa Mpwapwa. Kwa muktadha huo, ujenzi wa kuimairisha kingo hizo utaanza baada ya tathmini ya kina kukamilika.
Mheshimiwa Spika, Kupitia Bunge lako Tukufu ninaomba kutoa wito kwa halmashauri zote nchini kuendelea kusimamia kikamilifu Sheria ya Usimamizi wa Mazingira Sura 191 ili kuzuia shughuli za kibinadamu na kuelimisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira ili kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved