Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, upi mkakakati wa Serikali kukarabati barabara za pembezoni Tabora Mjini?

Supplementary Question 1

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyomngeza. Kwanza, ninaipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan. Sisi Tabora Mjini kwa kweli ndiyo maana tunaitwa Toronto, miundombinu yetu mingi imekuwa ni mizuri yakiwemo madaraja makubwa mawili yamekamilika. Katika kata ya Kabila (Daraja la Igombe) limekamilika na Ifucha pia tunaishukuru sana Serikali.

Mheshimiwa Spika, nina swali moja tu la nyongeza. Baada ya mvua hizi kunyesha kuna miundombinu mingi Tabora ambayo imeharibika sana. Ukianzia Kata ya Misha, ukipita Masagala mpaka unatokea Kata ya Mapambano, lakini unapokwenda Mzunguko kuanzia Kata ya Mtendeni, unaenda Kata ya Uyui, Kata ya Kakola mpaka Ikomwa kutokea Kabila barabara hizo sehemu nyingine hazipitiki kabisa.

Je, Serikali ina mkakati gani wa dharura wa Serikali kuhakikisha barabara hizi zinapitika katika kipindi hiki?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba kumjibu Mheshimiwa Mwakasaka; kwamba kama nilivyojibu kwenye majibu ya msingi kwamba, katika mwaka huu wa fedha 2024/2025 shilingi milioni 703.7 zimetengwa kwa ajili ya kufanya ukarabati kwenye barabara hizi kwenye barabara hizi katika kata alizozitaja.

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zinatarajia kufikia kilometa 61; pia kujenga box karavati mbili na ujenzi wa karavati za mduara 20 kwenye kata ikiwemo Uyui, Tumbi, Kabila, Ikomwa, Ifucha, Ntalikwa, Itonjanda pamoja na Ndevelwa. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kwamba, Serikali inaendelea na utekelezaji wa ujenzi na ukarabati wa barabara katika maeneo haya.

Mheshimiwa Spika, tunatambua kwamba mvua nyingi ambazo zimekuwa zikinysha zinaleta madhara na kuna baadhi ya maeneo ambayo mawasiliano yanakatika. Ndiyo maana Serikali ya Awamu ya Sita katika bajeti ya mwaka huu 2024/2025 imetenga bajeti ya ya dharura ya shilingi bilioni 71 ambayo hiyo inatumika kurudisha mawasiliano katika maeneo ambayo mawasiliano yamekatika kabisa. Kwa hiyo, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inatambua mazingira yanayojitokeza na hata mazingira ambayo yanajitokeza katika Jimbo lako la Tabora Mjini tunachukua hatua za dharura kuhakikisha tunafikia maeneo kama uliyoyajataja kwa ajili ya kuhakikisha tunarudisha mawasiliano ili wananchi waweze kutumia barabara hizi ambazo zinawanufaisha kiuchumi, lakini zinawasaidia kufika katika huduma za msingi za kijamii. Tutaendelea kufanya hivyo.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, upi mkakakati wa Serikali kukarabati barabara za pembezoni Tabora Mjini?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Barabara ya Mtandika – Msosa kilomita 16 ambayo ipi Ruaha Mbuyuni katika Wilaya ya Kilolo, hii barabara kwa kweli ina changamoto kubwa na imekata mawasiliano: -

Je, Serikali iko tayari sasa kurekebisha zile sehemu ambazo zimekatika mawasiliano ili iweze kupitika?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, inafanya uwekezaji mkubwa sana katika kuimarisha barabara hizi za Wilaya zinazosimamiwa na TARURA. Ndiyo maana tutaona kwamba katika kipindi cha Awamu ya Sita bajeti ya TARURA imeongezeka maradufu. Hapo mwanzo bajeti ya TARURA kila mwaka ilikuwa ni bilioni 275, lakini tunavyozungumza tunatarajia katika mwaka wa fedha 2025/2026 bajeti ya TARURA itakuwa ni trilioni 1.8.

Mheshimiwa Spika, vilevile, ukiacha bajeti hiyo tu kunakuwa na bajeti ya dharura. Mathalani, katika mwaka huu wa bajeti tuna bilioni 71 kama bajeti ya dharura. Kazi kubwa ya bajeti hii ya dharura ni kufanya au kuchukua hatua za dharura kurudisha mawasiliano kwenye maeneo ambayo barabara zimekata mawasiliano ili wananchi waweze kuzitumia.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ninaomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, niweze kumwagiza Meneja wa TARURA Mkoa wa Iringa, pamoja na wa wilaya waweze kufuatilia babaara hii ya Mtandika – Msosa aliyoitaja Mheshimiwa Ritta Kabati, na waweze kuiweka katika mpango kwa ajili ya kuhakikisha kwamba mawasiliano yanarejeshwa ili wananchi waweze kuitumia barabara hii ambayo inawanufaisha kiuchumi, lakini itawasaidia kufikia huduma za msingi za kijamii.

Name

Kenneth Ernest Nollo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bahi

Primary Question

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: - Je, upi mkakakati wa Serikali kukarabati barabara za pembezoni Tabora Mjini?

Supplementary Question 3

MHE. KENNETH E. NOLLO: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Box karavati ya Mayamaya – Mpondali iko kwenye package ya Miradi ya kuendeleza miji na tayari mkandarasi amepatikana: -

Je, ni lini Mkandarasi atafika site kuanza kazi ya ujenzi wa box karavati hiyo?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Spika, ninaomba nitumie nafasi hii kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI kumkumbusha wajibu wa msingi Meneja wa TARURA wa Mkoa wa Dodoma pamoja na Meneja wa TARURA Wilaya ya Bahi kuhakikisha kwamba Mkandarasi huyu aliyepatikana anaweza kukabidhiwa kazi (site) na aweze kuanza kutekeleza Mradi huu kwa mujibu wa ratiba ya kazi ambayo ipo katika mkataba.