Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 320 2025-05-15

Name

Emmanuel Adamson Mwakasaka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tabora Mjini

Primary Question

MHE. EMMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza: -

Je, upi mkakakati wa Serikali kukarabati barabara za pembezoni Tabora Mjini?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2023/2024, shilingi milioni 585.2 zilitumika kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 46.6, ujenzi wa kalavati 4 za box, ujenzi wa kalavati 10 za mduara, ukarabati wa daraja moja na ujenzi wa mitaro mita 500 za urefu katika kata za Ikomwa, Ifucha, Itetemia, Uyui, Misha, Itonjanda na Ndevelwa.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2024/2025, zimetengwa shilingi milioni 703.7 ambapo kazi za kukarabati barabara zenye urefu wa kilomita 61, ujenzi wa kalavati 2 za box, ujenzi wa kalavati 20 za mduara katika kata za Uyui, Tumbi, Kabila, Ikomwa, Ifucha, Ntalikwa, Itonjanda na Ndevelwa zimekwishaanza kufanyika na zinatarajiwa kukamilika ifikapo Julai 2025.

Mheshimiwa Spika, serikali itaendelea kuihudumia miundombinu ya barabara na madaraja zikiwemo barabara za pembezoni mwa Mji wa Tabora kwa kuzijenga, kuzikarabati na kuzifanyia matengenezo kulingana na upatikanaji wa fedha.