Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, lini Zahanati za Buhulyu, Mogwa, Mwanzilwo na Gulyambi - Bukene zitaanza kutoa huduma?

Supplementary Question 1

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba, Zahanati za Buhulyu, Mogwa na Gulyambi zimekamilika na zinaanza kutoa huduma. Hata hivyo nimezitembelea hizi zahanati zote.

Mheshimiwa Spika, kuna changamoto kubwa kwamba zote hizi hazina bajeti yake ya dawa; na wanalazimika kuazima tu dawa chache kutoka zahanati za jirani. Wao kwanza hawana dawa za kutosha na zile zahanati za jirani wanazipunguzia dawa. Je, Serikali wana mpango gani, kwamba hizi zzhanati zinapoanza kutoa huduma ziwe zimekamilika na ziwe na bajeti yake yenyewe ya dawa badala ya kuanza kwa kuazima azima dawa chache kutoka zahanati za jirani?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Katika ujenzi wa zahanati na vituo vya afya, kwa kawaida pale ambapo tunaweka maoteo ya ukamilishaji wa majengo hayo na kuanza kutoa huduma, halmashauri ina wajibu kupitia Mganga Mkuu wa Halmashauri, pamoja na Mganga Mkuu wa Mkoa kupeleka taarifa mapema Bohari kuu ya Dawa (MSD) ili iweze kuwekwa kwenye orodha ya vituo ambavyo vinahitaji kupata dawa mara baada ya kusajiliwa.

Mheshimiwa Spika, ikiwa imekamilika katikati ya mwaka wa fedha, mara nyingine inakuwa na changamoto ya kuingizwa kwenye mfumo wa dawa kwa sababu bajeti yake inaingizwa mwaka unaofuata wa fedha.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Selemani Jumanne Zedi, kwamba, tumefanya hivyo ili angalau wananchi katika maeneo haya waanze kupata za afya za msingi. Mwaka ujao wa fedha, kwa maana ya mwezi ujao Julai tutahakikisha kuwa zahanati hizi zinaingia kwenye bajeti, lakini pia zinaingia kwenye mfumo wa MSD ili zianze kupokea dawa hizo kwa mujibu wa taratibu.