Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 586 2025-06-16

Name

Selemani Jumanne Zedi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukene

Primary Question

MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: -

Je, lini Zahanati za Buhulyu, Mogwa, Mwanzilwo na Gulyambi - Bukene zitaanza kutoa huduma?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kujenga vituo vya kutolea huduma na kuvisajili ili vianze kutoa huduma za afya. Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2024/2025 jumla ya zahanati 1,158 zimejengwa na kusajiliwa na zinatoa huduma.

Mheshimiwa Spika, Zahanati ya Buhulyu, Mogwa na Gulyambi zimekamilika, zimesajiliwa na zinatoa huduma. Aidha, Zahanati ya Mwanzwilo ujenzi umefikia hatua ya ukamilishaji 80% ambapo Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Nzega imetenga shilingi milioni 30 katika mwaka wa fedha 2025/2026 kwa ajili ya ukamilishaji.