Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Joseph Michael Mkundi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ukerewe
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. DANIEL T. AWACK aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Wodi ya Wazazi na Jengo la Maabara Kituo cha Afya Oldeani Karatu?
Supplementary Question 1
MHE. JOSEPH M. MKUNDI: Mheshimiwa Spika, ninashukuru. Ninaipongeza Serikali kwa tathmini hiyo na hatua waliyoifanya. Hata hivyo, nilitaka kujua, swali langu la kwanza; kwa kuwa tayari tathmini imefanyika, sasa kuna mpango gani wa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Karatu ili kuona kwamba maeneo yote ambayo ni chakavu na yana changamoto kama hizo kwenye Jimbo la Karatu, basi vituo hivyo vinafanyiwa marekebisho?
Mheshimiwa Spika, kwenye Jimbo la Ukerewe kuna Kituo cha Afya cha Nakatunguru ambacho kilijengwa mwaka 2012 na kina upungufu mkubwa sana wa majengo kiasi kwamba baadhi ya huduma zinashindwa kufanyika kwa sababu ya miundombinu kutokuwa kamilifu. Je, ni lini sasa Ofisi ya Rais, TAMISEMI watasaidia kukamilisha majengo kwenye kituo hiki cha afya ili wananchi waweze kupata huduma stahiki kwenye kituo hicho?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge Joseph Mkundi, kwa niaba ya Mheshimiwa Daniel Tlemai Awack, kwamba, Serikali ilishafanya tathmini ya majengo na uchakavu wa Kituo cha Afya cha Oldeani, na tayari tumeanza kutenga fedha kwa ajili ya ukarabati wa majengo ikiwemo Jengo la huduma ya kujifungulia.
Mheshimiwa Spika, mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya shilingi milioni 20 zimepelekwa kwa ajili ya ukarabati. Vilevile, mwaka ujao wa fedha, mapato ya ndani, shilingi milioni 28 zimetengwa kwa ajili ya kuanza ujenzi wa jengo la upasuaji. Kwa hiyo, haya yanafanyika wakati Serikali Kuu ikiandaa fedha kwa ajili ya kwenda kufanya upanuzi na ukarabati mkubwa wa kituo hiki cha afya.
Mheshimiwa Spika, kuhusiana na hoja ya pili kuhusu Kituo cha Afya cha Nakatunguru katika Jimbo la Ukerewe, ni kweli kwamba, Serikali ilipeleka fedha mwaka 2012 na kituo cha afya kimejengwa na kimeanza kutoa huduma.
Mheshimiwa Spika, vituo hivi vya afya tunavijenga kwa awamu. Huu ujenzi ulikuwa ni wa awamu ya kwanza. Sasa tunakwenda kuandaa mpango kwa ajili ya ujenzi wa awamu ya pili ili kukamilisha majengo ambayo yamesalia. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mkundi kwamba Serikali inalitambua hilo na tayari imeweka mpango kwa ajili ya kwenda kumalizia majengo yaliyobaki katika awamu ya pili.
Name
Tumaini Bryceson Magessa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busanda
Primary Question
MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. DANIEL T. AWACK aliuliza: - Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Wodi ya Wazazi na Jengo la Maabara Kituo cha Afya Oldeani Karatu?
Supplementary Question 2
MHE. TUMAINI B. MAGESA: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Kituo cha Afya Chikobe kilijengwa mwaka 1976. Hali yake ya utendaji kwa sasa siyo bora tena. Je, ni lini Serikali itafanya uboreshaji ili kiweze kuwahudumia wananchi vizuri zaidi?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Chikobe, kimewekwa kwenye Mpango wa Benki ya Dunia Awamu ya Pili, ambapo tunatarajia mwaka ujao wa fedha 2025/2026 tutapeleka fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati na kuongeza majengo katika Kituo cha Afya cha Chikobe.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved