Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 585 2025-06-16

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. JOSEPH M. MKUNDI K.n.y. MHE. DANIEL T. AWACK aliuliza: -

Je, lini Serikali itatoa fedha za ujenzi wa Wodi ya Wazazi na Jengo la Maabara Kituo cha Afya Oldeani Karatu?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Oldeani kilichopo katika Kata ya Oldeani, Halmashauri ya Karatu, kilijengwa mwaka 1971. Kituo hicho kina upungufu na uchakavu wa baadhi ya majengo yakiwemo Wodi ya Wazazi, Jengo la Kuhudumia Wagonjwa wa Nje (OPD), Jengo la Upasuaji, Jengo la Wazazi, Jengo la Maabara na Jengo la Huduma za Baba, Mama na Mtoto (RCH).

Mheshimiwa Spika, ili kuboresha miundombinu ya kituo hicho, Serikali imekiingiza kwenye orodha ya vituo vya afya kongwe 203 ambavyo Serikali ilivifanyia tathmini kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu yake.

Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha ukarabati wa hospitali 50 kongwe nchini, na baada ya hapo itafanya ukarabati wa vituo vya afya na zahanati kongwe kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya cha Oldeani Karatu.