Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zaytun Seif Swai

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. ZAYTUN S. SWAI: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; wananchi wa Ngorongoro bado wanataka kufahamu ni lini Barabara ya kutoka Wasso hadi Loliondo ujenzi wa lami utakamilika?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; wananchi wa Wilaya ya Monduli wamesubiria kwa muda mrefu sana barabara ya kutoka Kigongoni - Selela hadi Engaruka ni barabara yenye urefu wa kilometa 26 kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Chama Cha Mapinduzi. Je, ni lini ujenzi wa barabara hii utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu lini itakamilika hii Barabara ya Wasso kwenda Loliondo, tumesema tumeshasaini na baada ya kusaini tunategemea mkandarasi aanze kazi. Tutakachohakikisha ni kwamba tunamsimamia huyo mkandarasi ili aweze kukamilisha kipande hicho kwa muda na kuhusu barabara aliyoitaja ni kwamba tuna vipande kadhaa ambavyo tuna Mto wa Mbu hadi Selela, Selela hadi Engaruka na Engaruka hadi Ngare Sero.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge vipande vyote hivi viko kwenye utaratibu wa kuanza kuvijenga kwa kiwango cha lami na yalikuwa ni maelekezo ya Viongozi wa Kitaifa, lakini pia kama Serikali tumeipangia katika mwaka huu iweze kutangazwa na kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Ahsante.

Name

Shally Josepha Raymond

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 2

MHE. SHALLY J. RAYMOND: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya kutoka Rau - Shimbwe na Rau – Kinyamvuo kupitia Mamboleo ni ahadi za Viongozi Wakuu wa Kitaifa kwa awamu tatu mfululizo. Leo tunataka kufahamu ni lini barabara hiyo itaanza kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge ahadi za Viongozi na hasa wa Kitaifa huwa ni kipaumbele. Hivyo, nimhakikishie kwamba TANROADS pamoja na wenzetu wa TARURA tutahakikisha kwamba ahadi za hawa viongozi zinatekelezwa ili wananchi hawa waweze kupata huduma ya barabara za kiwango cha lami kama zilivyokuwa zimeelekezwa na Viongozi wetu wa Kitaifa. Ahsante.

Name

Esther Nicholus Matiko

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Utegi – Shirati mpaka Kirongwe ambayo inaunganisha upande wa Kenya ni barabara ya muda mrefu sana tangu Awamu ya Tatu ya Mheshimiwa Mkapa. Je, ni lini sasa Serikali itaweza kukamilisha kipande hiki cha lami ambacho ni muhimu sana kwa uchumi wa Mara? Ahsante. (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tunavyoongea hii barabara tulishaitangaza, kwa hiyo iko kwenye hatua za manunuzi. Ahsante.

Name

Innocent Edward Kalogeris

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 4

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS: Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara ya Ngerengere – Mvuha kwenda Kisaki hadi Mtemele Junction ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami umefikia wapi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa hii barabara tutafanya mapitio, lakini kwa maana ya Mvuha kuja Bigwa tulishasaini mkataba, tunasubiri malipo ya advance ya mkandarasi hizo kilometa 78. Ahsante.

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 5

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Moshi – Arusha tuliambiwa mkandarasi amesharipoti, lakini mpaka sasa hivi hatumwoni site na alitakiwa awe ameanza kulipa fidia wananchi kupisha Daraja la Kikafu. Je, ni lini tutamwona kwa macho mkandarasi akiwa site? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, labda tu niseme kwamba hiyo barabara ambayo tunasaidiana na wenzetu wa JICA inafanyiwa mapitio upya pamoja na kupatikana kwa mkandarasi, lakini imelazimika kuwe na mapitio upya ya usanifu ili iendane na hizo njia nne ikiwa ni pamoja na hilo Daraja la Kikafu. Tunaamini muda si mrefu ujenzi wa barabara hii utaanza ambapo ni kutoka Arusha – Kikafu pamoja na barabara za Mji wa Moshi.

Name

Shamsia Aziz Mtamba

Sex

Female

Party

CUF

Constituent

Mtwara Vijijini

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 6

MHE. SHAMSIA A. MTAMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itakamilisha barabara ya lami ambayo inakwenda kwenye Halmashauri yetu Naguruwe – Mkunwa na Hiyari – Mkunwa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara zote za TANROADS mipango yake ni kuwa barabara za kiwango cha lami, lakini barabara zote haziwezi kujengwa kwa wakati mmoja ikiwa ni pamoja na hiyo, lakini nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, kadri Serikali itakavyokuwa inapata hela basi hiyo barabara tutaijenga na hasahasa kama inakwenda kwenye makao makuu ya halmashauri. Ni moja ya vipaumbele vya Serikali kuunganisha makao makuu ya mikoa na halmashauri ama makao makuu ya wilaya. Ahsante.

Name

Timotheo Paul Mnzava

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Korogwe Vijijini

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:- Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Supplementary Question 7

MHE. TIMOTHEO P. MNZAVA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuelezwa kwamba mkandarasi wa kujenga Barabara ya Soni – Bumbuli – Dindira – Korogwe ameshapatikana, lakini mpaka leo kuna ukimya. Mheshimiwa Waziri ni lini mkataba utasainiwa ili mkandarasi aende kazini akafanye kazi ya kuwajengea barabara watu wa Korogwe na wa Bumbuli? Ninakushukuru.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, tunachosubiri kwa kweli ni malipo ya awali ya huyo mkandarasi ili aweze kusaini na kuanza kazi. Ahsante.