Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 546 2025-06-09

Name

Emmanuel Lekishon Shangai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ngorongoro

Primary Question

MHE. ZAYTUN S. SWAI K.n.y. MHE. EMMANUEL L. SHANGAI aliuliza:-
Je, lini ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kutoka Wasso hadi Loliondo kilomita 10 utaanza?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Wasso hadi Loliondo yenye urefu wa kilomita 10 ni sehemu ya Barabara ya kutoka Mto wa Mbu hadi Loliondo yenye urefu wa kilometa 217. Serikali tayari imeanza taratibu za ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii kwa kuanza na sehemu ya Wasso hadi Loliondo yenye urefu wa kilometa 10 ambapo mkataba wa ujenzi umesainiwa tarehe 5 Juni, 2025 na taratibu za kuanza kazi za ujenzi zinaendelea. Kwa sehemu iliyobaki, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi. Ahsante.