Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Dorothy George Kilave
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Temeke
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 1
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, lakini ukiangalia sana, barabara hii ni muhimu sana kwa sababu inakwenda mpaka Mloganzila kwenye kituo cha afya. Je, hawaoni kwamba iko haja ya kumaliza haraka hizi kilomita 1.7 zilizobaki?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Je, TANROADS hawaoni kwamba sasa iko haja kubwa ya kuanza barabara ambayo inaanzia Sudan Jimboni Temeke mwisho kuelekea kwenda Soko Kuu la Tandika mkabala na Police Post ya Tandika, kwa sababu barabara hii ni muhimu sana kwa kuwa inapitisha magari makubwa ambayo sidhani kama TARURA wana uwezo nayo; ili magari yale makubwa yanapopita yanapoleta bidhaa kutoka mikoani iwe sahihi kwa sababu sasa hivi imebomoka sana?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua hii barabara ilivyo na umuhimu. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba leo nimepata taarifa kuwa mkandarasi tayari ameshapatikana kukamilisha hizo kilomita 1.7. Pia barabara hiyo tumeitengea fedha kwa mwaka ujao wa fedha. Hii ninayosema ni kwa mwaka huu, lakini pia imetengewa fedha katika mwaka ujao wa fedha.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu hii Barabara ya Sudan – Soko Kuu la Tandika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, sisi pamoja na wenzetu wa TARURA tutasaidiana kuhakikisha kwamba tunaupa umuhimu wa aina yake ili kwanza iweze kukarabatiwa, lakini pia kuijenga vizuri kulingana na hadhi na eneo lenyewe na magari yenyewe yanayopita hapo, ahsante.
Name
Joseph Anania Tadayo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwanga
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 2
MHE. JOSEPH A. TADAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kuniona. Je, ni lini Serikali itakamilisha kwa kiwango cha lami barabara ya Mwanga – Kikweni – Kifula – Vuchamangofi?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara hii imekuwa ikijengwa kwa awamu na tuko hatua za mwisho. Mkandarasi yuko ambaye anaendelea kilomita hizo tatu, lakini bado kilomita tano ambazo zimepangwa kujengwa katika mwaka wa fedha ujao. Hivyo nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba barabara hiyo kwa mwaka ujao kutoka Kikweni hadi Vuchamangofi itakuwa imekamilika kwa hizo kilomita tano ambazo zimebaki.
Name
Priscus Jacob Tarimo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Mjini
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 3
MHE. PRISCUS J. TARIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana. Barabara ya Mabogini – Kahe iko chini ya TARURA, lakini ilishaombewa kuja TANROADS ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami. Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi hii?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara ikishapandishwa hadhi, ikishakuja kwetu, ndiyo tunapangiwa bajeti; lakini kama tutakuwa tumechukua maana yake bajeti ambayo ilikuwa imepangiwa TARURA tutaendelea kutekeleza kwa bajeti hiyo hiyo ya TARURA. Kwa upande wa TANROADS wakati sasa itakapokuwa tunaipangia bajeti, tutaipanga kwa utaratibu wa TANROADS na kama inatakiwa ifanyiwe usanifu upya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, niwahakikishie Waheshimiwa Wabunge kwamba changamoto ambayo tumekuwa tunaipata wakati mwingine ni pale ambapo hadhi ya barabara za TARURA zinakuwa na upana wa mita 30, lakini zinapokuja TANROADS tunatakiwa tuongeze. Hapo ndipo panapokuwa na changamoto.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tunaweza tukaichukua moja kwa moja ama tukakasimiwa kuendelea kuifanyia matengenezo lakini ikiwa kwenye vipimo vilevile vya TARURA wakati tunaandaa fedha ya kulipa hizo mita 60, ahsante.
Name
Mariamu Nassoro Kisangi
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 4
MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Je, Serikali ina mpango gani wa dharura wa kuziba mashimo katika eneo la Vetenari Makutano na Barabara ya Mandela ambapo hali ya eneo hilo ni mbaya sana, na kwamba magari yanashindwa kupita?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, barabara aliyoitaja ni kati ya barabara kubwa katika Mji wa Dar es Salaam. Nitoe maelekezo kwa Meneja wa Mkoa wa Dar es salaam aende akafanye tathmini, na hiyo kazi ya kuziba hayo mashimo iweze kufanyika kwa uharaka unaowezekana, ahsante.
Name
Boniphace Nyangindu Butondo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kishapu
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 5
MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru sana. Barabara ya Kolandoto kwenda Munze hadi Mwangongo kilomita 63 katika kiwango cha lami, waliahidi kuwa watatekeleza mwaka wa fedha uliopita. Je, ni lini sasa utekelezaji wa mradi huu utaanza kufanyika?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli tulipanga kutekeleza hiyo Barabara ya Kolandoto – Mwangongo, na ndiyo barabara inayoenda Lalagwa hadi Sibiti. Tutaanza kujenga na tulishasaini mkataba Lalago kwenda Nkamo, lakini kwa upande wa Mwangongo hadi Kolandoto tumeendelea kuitengea fedha hata mwaka ujao wa fedha ili tuweze kujenga kipande hicho.
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:- Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?
Supplementary Question 6
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Wilaya ya Kyerwa ni moja kati ya wilaya ambayo haina kilomita hata moja ya lami. Sasa ninataka kujua, je, ni lini Barabara zetu za Omugakorongo kwenda Murongo pamoja na Bugene kwenda Kaisho zitaanza kujengwa?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, tuna barabara tatu ambazo ziko kwenye mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami katika Wilaya ya Kyerwa. Kwanza ni Omurushaka kwenda Nkwenda ambapo mkandarasi tulishampata, Omugakorongo kwenda Murongo tayari iko kwenye manunuzi, pia Bugene – Burigi – Chato kwenda Kasumo mkandarasi yuko site akiwa anafanya kazi za ujenzi kwa kiwango cha lami.