Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 544 2025-06-09

Name

Issa Jumanne Mtemvu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kibamba

Primary Question

MHE. DOROTHY G. KILAVE K.n.y. MHE. ISSA J. MTEMVU aliuliza:-

Je, lini Serikai itakamilisha ujenzi wa barabara kutokea Makondeko – Kwembe hadi Mloganzila?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia TANROADS imekuwa ikijenga barabara ya Makondeko – Kwembe – Mloganzila yenye urefu wa kilometa 17.26 kwa awamu, ambapo kilometa 4.89 zimejengwa kwa kiwango cha lami kuanzia Mloganzila – Kibamba.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali kupitia TANROADS imepanga kuendelea na ujenzi wa barabara hii kwa urefu wa kilometa 1.7. Kwa sasa mradi upo kwenye hatua za manunuzi ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza kazi za ujenzi, ahsante.