Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je, Serikali haioni ipo haja ya kupitia upya mikataba ya mashamba ya ushirika na kufanya tathmini ya ardhi ya mashamba hayo?

Supplementary Question 1

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali inaendelea kufanya tathmini kwenye mashamba haya, na kwa kuwa wananchi hawajashirikishwa, na kwa kuwa migogoro inaendelea kujitokeza kati ya wawekezaji na vyama vya msingi pamoja na wananchi, je, Serikali haioni kwamba ipo haja ya kusitisha kwanza kwa muda mkataba wa Chama cha Ushirika cha Fond; kwa maana ya For Nronga Warry ili kwanza tathmini hiyo ifanyike na mkataba uwe shirikishi ndipo mkataba huu uweze kusainiwa na kuepusha migogoro?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu la pili, kwa kuwa kumekuwa na migogoro mingi inayotokana na kutokushirikishwa kwa wadau wengi wanaohusika na ushirika na kuzalisha migogoro isiyokuwa na sababu, je, Serikali haioni kuwa ipo haja kwa mikataba hii kuhusishwa kwenye Wizara ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ili mikataba hii ipitiwe vizuri ili ikisainiwa iwe na tija kwa Serikali na kwa vyama vya ushirika?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mimi nimpongeze sana Mbunge wa Jimbo la Hai Mheshimiwa Mafuwe hususan kwa kupigania vyama vya ushirika katika jimbo lake kwa muda wote wa miaka mitano.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimthibitishie tu kwamba, moja ni kwamba tutaendelea kufanya tathmini, na nimeshawaelekeza Tume ya Ushirika, kwamba wasisaini mkataba wowote bila kuwashikirisha wananchi. Kwa hiyo, hata katika chama cha ushirika eneo la Fongo hicho cha Nronga Warry maelekezo ni hayo hayo, kwamba, wawashirikishe wananchi, wananchi waridhie ndipo mkataba huo uweze kusainiwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusiana na haja ya Serikali kushirikiana na Wizara ya Mipango na Uwekezaji pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni sehemu ya maelekezo ambayo tumeshapatiwa sasa hivi kuanza kuyapitia. Kwa hiyo, jambo hilo lipo katika mipango ya Serikali na tutaanza kulitumia katika mikataba yote inayofuata baada ya sasa, ahsante.