Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 542 2025-06-09

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, Serikali haioni ipo haja ya kupitia upya mikataba ya mashamba ya ushirika na kufanya tathmini ya ardhi ya mashamba hayo?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Maendeleo ya Ushirika inafanya mapitio na tathmini ya mikataba ya uwekezaji katika mashamba ya ushirika. Baadhi ya mikataba inayoendelea kufanyiwa mapitio ni ya mashamba ya Vyama vya Ushirika vya Miradi ya pamoja ya Kyumasha, Murososangi, Fonrwa, Lyamungo Amcos, Manush Narumu; Mashamba ya Vyama vya Ushirika vya Kilimaboro, Masama Mula, Kibosho Kati na Chama Kikuu cha Ushirika Kilimanjaro.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Tume ya Maendeleo ya Ushirika imeweka moduli ya uwekezaji kwenye Mfumo wa Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (MUVU) kwa lengo la kufanyiwa upembuzi na tathmini. Hadi sasa jumla ya mashamba 408 ya vyama vya ushirika yenye thamani ya shilingi bilioni 271.48 yameingizwa kwenye mfumo huo.