Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha zoezi la upimaji wa ardhi katika Halmashauri ya Kasulu DC?

Supplementary Question 1

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali moja la nyongeza. Kumekuwepo na migogoro ya mipaka kati ya vijiji na vijiji, wilaya na wilaya, mikoa na mikoa na Serikali ipo. Lini migogoro hii itaisha?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kwanza nampongeza Mheshimiwa Kavejuru kwa swali lake. Ni kweli kabisa migogoro ipo na tunaendelea kupambana kuipunguza, na siku moja itamalizika kabisa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, migogoro ya vijiji na vijiji, kupitia Tume yetu ya Mipango na Matumizi Bora ya Ardhi, ukweli imeonesha matokeo mazuri sana, na kwa sasa tunaendelea. Watu wako uwandani kwenye baadhi ya vijiji katika wilaya nyingi hapa nchini, kwa ajili ya kuweka mpango wa matumizi bora ya ardhi, ambao tumeona ni suluhisho la migogoro hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu migogoro kati ya wilaya na wilaya na mkoa na Mkoa, ni migogoro ya kiutawala. Mjue nchi yetu siyo mpya katika upimaji wa maeneo, isipokuwa kumekuwa na mgongano tu wa maeneo haya mawili kati ya wilaya moja na nyingine, na mkoa mmoja na mwingine. Tumeendelea na utatuzi katika kuwaelimisha watu umuhimu wa kuheshimu mipaka ambayo tayari ilikwishawekwa siku nyingi sana.

Name

Halima James Mdee

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha zoezi la upimaji wa ardhi katika Halmashauri ya Kasulu DC?

Supplementary Question 2

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa hivi kuna zoezi la upimaji na uuzaji wa viwanja linaloendeshwa na Shirika la Maendeleo Dar es Salaam (DDC) katika Halmashauri mbili za Ubungo na Kinondoni, zoezi ambalo lina ugomvi na mgogoro mkubwa sana. Waziri aliahidi mbele ya Bunge kwenda kutatua mgogoro kati ya tarehe 2 na 7 mwezi wa Sita, leo ni tarehe 9 Juni, Waziri hajaonekana. Naomba majibu ya Serikali, Waziri ataenda lini na/au tutaongozana naye lini?

Name

Deogratius John Ndejembi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chamwino

Answer

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nashukuru kwa jibu na ninampongeza Mheshimiwa Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri kwa maswali ambayo amekuwa akiyajibu hapa. Namhakikishia Mheshimiwa Mbunge Halima Mdee kwamba, hali yangu ya kiafya haikuwa nzuri wiki yote iliyopita. Kwa hiyo, sikupata nafasi ya kuweza kwenda, lakini nitakaa naye tupange tuweze kwenda, kama nilivyoahidi na sikuahidi hapa tu ndani ya Bunge lako Tukufu, niliahidi vilevile nilipokutana na wale wazee walipokuja katika Wizara ya Ardhi. Kwa hiyo, nitafika katika eneo hilo. (Makofi)

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: - Je, lini Serikali itakamilisha zoezi la upimaji wa ardhi katika Halmashauri ya Kasulu DC?

Supplementary Question 3

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kuna mgogoro mkubwa kati ya Kijiji cha Chilunda na Kijiji cha Lipupu. Je, Wizara iko tayari kumwelekeza Kamishna wa Ardhi, Mkoa wa Mtwara, kwenda katika vijiji hivyo, ili kutoa suluhu ya mgogoro huo?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Mheshimiwa Mhata nadhani baada ya kumaliza kujibu maswali haya, tukutane ili tuweze kuliangalia kwa ukaribu, lakini nikubaliane na wewe kumwelekeza Kamishna wa Mkoa aende mara moja kwenye eneo hili la mgogoro na baadaye tupate mrejesho wa pamoja wa chanzo cha mgogoro.