Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Lands, Housing and Human Settlement Development Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi 539 2025-06-09

Name

Josephine Johnson Genzabuke

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza: -

Je, lini Serikali itakamilisha zoezi la upimaji wa ardhi katika Halmashauri ya Kasulu DC?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2022/2023, Wizara ilitoa fedha kiasi cha shilingi milioni 50 kwa Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, kwa ajili ya kupanga, kupima na kumilikishwa viwanja 500 kupitia Programu ya Kupanga, Kupima na Kumilikisha Ardhi (KKK).

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kutumia fedha hizo, zaidi ya vipande vya ardhi 1,200 vilitambuliwa, viwanja 866 vimepimwa na kuidhinishwa katika Mitaa ya Nyangwa, Makere na Kalimungoma. Zoezi la kumilikisha viwanja 866 vilivyoidhinishwa linaendelea kupitia mazoezi ya Kliniki za Ardhi, Ofisi za Halmashauri na Ofisi ya Ardhi, Mkoa wa Kigoma, ambapo jumla ya Hatimilki 47 zimeandaliwa na kati ya hizo, 37 zimekabidhiwa kwa wananchi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, sambamba na zoezi la utambuzi na upimaji ardhi, kazi ya kuhuisha mipaka baina ya Vijiji vya Kagerankanda na Uvinza vilivyopakana na Msitu wa Hifadhi wa Makere Kusini pamoja na Kitalu cha Uwindaji ilifanyika, na pia, ukaguzi na uidhinishaji wa upimaji wa vijiji hivyo viwili unaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, eneo ambalo wananchi wa Kitongoji cha Katoto watahamishiwa kupisha eneo wanaloishi kwa sasa limetengwa, ikiwa ni utekelezaji wa uamuzi wa Baraza la Mawaziri kuhusu utatuzi wa migogoro katika vijiji/mitaa 975. Kadhalika, zoezi la urasimishaji makazi katika mitaa mbalimbali linaendelea, ambapo jumla ya viwanja 4,813 vimepimwa na kuidhinishwa katika Halmashauri ya Mji wa Kasulu.