Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 1

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Ninaomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa mkakati wa Serikali ulikuwa chuo hiki kingeweza kukamilika mapema na kuanza kudahili wanafunzi mwaka huu wa 2025, je, ni sababu zipi zilizopelekea zoezi hilo la ujenzi wa chuo hiki kuchelewa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili. Ningependa kujua mikakati ambayo Serikali inayo katika kuhakikisha kwamba mafunzo ya ufundi stadi yanayotolewa katika vyuo vyetu vya VETA yanakwenda sambamba na maendeleo ya teknolojia na sayansi hapa duniani?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kuhusu kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa chuo, kumetokana na changamoto ikiwemo upatikanaji wa fedha kwa wakati. Hata hivyo, idadi ya sasa tayari Serikali imeshatoa fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa chuo na kwamba ujenzi unatarajiwa kukamilika kama nilivyojibu kwenye swali la msingi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili juu ya namna ya kuandaa mafunzo yanayoendana na teknolojia ya sasa; katika kuhakikisha mafunzo yanatolewa na vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi yanayoendana na maendeleo ya mabadiliko ya teknolojia, Serikali imefanya maboresho ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 23, pamoja na maboresho ya mitaala, ili kuhakikisha mafunzo yanazingatia maendeleo ya mabadiliko ya teknolojia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, mitaala yote iliyoboreshwa na ambayo inatumika katika vyuo vya mafunzo ya ufundi stadi imeweka mazingira ya kuhakikisha maendeleo ya mabadiliko na teknolojia yanapewa nafasi.

Name

Hussein Nassor Amar

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nyang'hwale

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 2

MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa, Serikali ilishaamua kutujengea Chuo cha Ufundi Stadi (VETA), Wilaya ya Nyang’wale, leo ni zaidi ya miaka minne chuo hicho hakijakamilika. Je, Serikali itakamilisha lini ujenzi wa chuo hicho cha VETA?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza nampongeza Mheshimiwa Mbunge wa Nyang’wale kwa ufuatiliaji wake kuhusu ukamilishaji wa Chuo cha VETA cha Nyang’wale. Namwahidi tu Mheshimiwa Mbunge kwamba, baada ya kupitisha bajeti yetu ya Wizara ya Elimu, Serikali inakwenda kukamilisha vyuo vyote ambavyo viko kwenye progress ya ujenzi na Nyang’wale ikiwemo.

Name

Deodatus Philip Mwanyika

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Njombe Mjini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:- Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Kilwa?

Supplementary Question 3

MHE. DEODATUS P. MWANYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi. Halmashauri ya Mji Njombe tuliahidiwa kujengewa Chuo cha VETA na eneo lilitengwa, lakini hatupo katika mpango huo. Nini mpango wa Serikali kujenga vyuo vya VETA kwenye halmashauri za miji ambazo tayari zina uhitaji mkubwa?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, tunajua ukweli kabisa kwamba, umuhimu wa VETA kwa nchi yetu ni mkubwa sana. Ndiyo maana Dkt. Mama Samia Suluhu Hassan, Rais wetu, ameweza kutoa fedha nyingi za ujenzi wa vituo hivi vya VETA katika wilaya mbalimbali na kwa sasa tunakwenda kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamwahidi Mheshimiwa Mwanyika kwamba, katika awamu inayofuata baada ya hii ya kwanza, ambayo fedha zimetolewa kwenda kwenye site, na Njombe itakuwemo.