Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 538 2025-06-09

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilaya ya Kilwa?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Chuo cha Ufundi Stadi cha Wilaya ya Kilwa ni miongoni mwa Vyuo 64 vya VETA vinavyojengwa na Serikali katika Wilaya ambazo zilikuwa hazijajengewa Vyuo vya Ufundi Stadi pamoja na Chuo kimoja cha Mkoa wa Songwe ambao ulikuwa hauna Chuo cha VETA cha Mkoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, awamu ya kwanza ya ujenzi wa Chuo cha VETA cha Wilaya ya Kilwa unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 1.6 ambapo hadi sasa kiasi cha shilingi 682,881,780.24 kimetumika. Aidha, ujenzi wa Chuo hiki umefikia 40% na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2025.