Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:- Je, lini Serikali italeta marekebisho ya Sheria ya Ndoa kuhusu ndoa ya jinsia moja au Muswada wa Sheria kupiga marufuku ndoa ya jinsia moja?

Supplementary Question 1

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza, kumekuwa na ongezeko kubwa la ndoa za utotoni na kumekuwa na unyanyasaji wa hawa watoto ambao wanaolewa wakiwa wadogo. Serikali mna mkakati gani wa kukomesha ndoa za utotoni? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kumekuwa na manyanyaso sana ya wanawake kupigwa na kunyanyaswa wakiwa kwenye ndoa. Je, mmefanya utafiti wa kutosha kuona hayo manyanyaso yapo makubwa kiasi gani? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu ndoa za utotoni kukomeshwa, ni kweli matukio haya yapo katika baadhi ya maeneo, lakini yanadhibitiwa kwa sheria mbalimbali ikiwepo Sheria ya Mtoto inayozuia mtoto kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji, unyanyasaji ikiwa ni pamoja na ndoa za utotoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, tuna imani sheria hiyo ikisimamiwa vyema ikiwa ni pamoja na wananchi kuielewa na kuchukua hatua za kutoa taarifa kwenye vyombo vya usimamizi wa sheria ili hatua stahiki zichukuliwe ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani, then tutakuwa tumesaidia kukomesha jambo hilo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, jambo la muhimu kuliko yote ni wananchi wa Tanzania kuzingatia maadili, mila, na desturi zetu ambazo zinazuia mtoto kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji ili hatimaye tuwe na kizazi ambacho kipo katika malezi yaliyo bora zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu manyanyaso ya wanawake kupigwa ni jambo ambalo limepigiwa kelele mara nyingi na sheria zetu za jinai haziruhusu, na siyo mwanamke tu, bali hata mtu yeyote kupigwa. Kwa hiyo, inapotokea mwanamke kapigwa kwa sababu tu ya kuwa katika ndoa, sheria zinaruhusu mwanamama huyu kulalamika katika vyombo vya usimamizi wa sheria ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya wanaume wanaokiuka misingi bora ya ndoa zetu ikiwa ni pamoja na kuepuka kuwapiga wake zetu, ahsante.

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:- Je, lini Serikali italeta marekebisho ya Sheria ya Ndoa kuhusu ndoa ya jinsia moja au Muswada wa Sheria kupiga marufuku ndoa ya jinsia moja?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru, lakini umesahau jina langu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maoni yale yaliyokusanywa na tukapewa muda kama mwaka mzima (mwaka jana), ni lini sasa mtaleta ile Sheria ya Ndoa hapa Bungeni? Ule Muswada mtauleta lini? (Makofi)

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu katika jibu la msingi la swali husika nimesema Serikali ipo katika hatua za mwisho za kukamilisha kuandaa Muswada wa marekebisho ya sheria mbalimbali za Haki Jinai na swali kama anavyouliza Mheshimiwa Mbunge, (Dkt. Thea Ntara) litazingatiwa ipasavyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru.