Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Justice and Constitutional Affairs Wizara ya Katiba na Sheria 537 2025-06-09

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. ESTER A. BULAYA K.n.y. MHE. NOAH L. S. MOLLEL aliuliza:-

Je, lini Serikali italeta marekebisho ya Sheria ya Ndoa kuhusu ndoa ya jinsia moja au Muswada wa Sheria kupiga marufuku ndoa ya jinsia moja?

Name

Sagini Jumanne Abdallah

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Butiama

Answer

NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa Kifungu cha Tisa cha Sheria ya Ndoa, Sura ya 29, ndoa imetafsiriwa kuwa makubaliano ya hiari kati ya mwanamke na mwanaume kuishi pamoja na inaweza kuwa ya mume mmoja na mke mmoja au mume mmoja na wake zaidi ya mmoja. Hivyo, sheria yetu haitambui ndoa ya aina nyingine yoyote isipokuwa kama ilivyotafsiriwa katika sheria tajwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kutekeleza mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai ambapo tupo katika hatua za mwisho za kukamilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali za Haki Jinai (The Criminal Justice (Miscellaneous Amendment) Bill) ambapo Kifungu cha 176 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16 kimependekezwa kufanyiwa marekebisho ili kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa maadili ikiwemo vitendo vya ndoa za jinsia moja, ninashukuru.