Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwanza ninaishukuru Serikali kwa kutujibu vizuri swali letu wananchi wa Wilaya ya Kilwa, lakini ningependa kuiomba Serikali iharakishe mchakato huo kutokana na umuhimu wa zoezi hili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ningependa kuuliza swali moja la nyongeza kwamba ni lini Mheshimiwa Waziri atafika Kilwa ili kuweza kushuhudia hali halisi ilivyo katika Mji wa Kivinje?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nichukue fursa hii kwanza nimshukuru na kumpongeza sana Mheshimiwa kwa niaba, lakini nimwambie tu kwamba kwanza tumeshaanza mchakato wa uandikaji wa miradi kwa ajili ya kuomba fedha hizi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, mchakato huu the way tutakapozipata fedha ndivyo ambavyo tutafanya haraka katika kuja kuanza angalau ujenzi; na kwa sababu tayari tumeshaanza tathmini ya awali, maana yake nimwombe tu Mheshimiwa kwa niaba ya wananchi wa Kilwa aendelee kuwa na Subira, mchakato huu umeshaanza na tutajitahidi tuharakishe.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili jambo la kwenda Kilwa nimwambie tu kwamba Serikali ya Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ipo tayari na inafikia wananchi wote wa Tanzania ili kuona namna ambavyo tunatatua changamoto zinazowakabili wananchi zikiwemo hizi changamoto za maji ya bahari kuingia katika maeneo ya makazi na vipando visivyo stahimili maji ya chumvi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu kwamba tupo tayari kwenda Kilwa kuona hali ilivyo na kuona namna ambavyo tunaweza tukawashauri na kuwasaidia wananchi, ninakushukuru.

Name

Asya Sharif Omar

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. ASYA SHARIF OMAR: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa kumekuwa na changamoto kubwa ya maji kutoka kwenye bahari na kuingia kwa wananchi kupelekea madhara mengi ambayo Mheshimiwa Waziri ameya-mention; ukuta wa Sepwese, Pemba umejengwa takribani sasa hivi ni mwaka wa tatu na wananchi bado wanaendelea kupata changamoto hizi. Tunataka kujua kauli ya Serikali, mradi huu utakamilika lini kwa upande wa Sepwese, Pemba ili kunusuru madhara kwa wananchi? (Makofi)

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimpongeze sana Mheshimiwa Asya kwani amekuwa mdau mzuri sana wa mazingira Zanzibar na maeneo mengine. Ninaomba nimwambie tu kwamba mara ya mwisho tulikwenda kwenye mradi wa Sepwese na kwa kweli tukakuta changamoto ya ule mradi haujakamilika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, nimwambie tu Mheshimiwa Asya kwamba hivi tunavyoongea, tayari mradi wa Sepwese wa ujenzi wa lile tuta umeshafikia 99% kwa maana kwamba ule mradi umeshakamilika. Kilichokuwa kinasubiriwa, ilikuwa ni sisi viongozi kama Wizara (Serikali) kwenda sasa kuwaambia wananchi na kuwakabidhi ule mradi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, pia, tukwambie, kabla hatujamaliza Bunge hili tutakwenda Sepwese tukakabidhi mradi ili sasa, wananchi waendelee kutumia na wanufaike na ule mradi ambao umejengwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan. Ninakushukuru sana.

Name

Simai Hassan Sadiki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nungwi

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Supplementary Question 3

MHE. SIMAI HASSAN SADIKI: Mheshimiwa Mwenyekiti, mara kwa mara nimekuwa nikisimama Bungeni hapa kuishauri Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania juu ya umuhimu wa ujenzi wa ukuta katika maeneo ya fukwe za bahari kule Nungwi. Je, nilichokuwa ninataka kufahamu, ujenzi ule umefikia wapi?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna maeneo mengi yamekuwa na changamoto hii ya maji ya bahari kutoka katika kina na kuingia kwenye makazi na kuingia kwenye vipando kama nilivyosema ambavyo havistahimili maji ya bahari. Changamoto hii ipo maeneo mengi; moja, ilikuwepo Sepwese ambayo tayari tumeshaikamilisha; ipo pia Gando, Mikindani, Lindi na maeneo mengine ambayo yanaingia maji ya bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie Mheshimiwa Simai kwamba kwanza ahadi hii tunaikumbuka na ndiyo maana kama atakumbuka katika bajeti ambayo tumeisoma hapa ya mwaka huu ya Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira katika zile shilingi bilioni 89 ambazo tumeidhinishiwa na Bunge hili tumesema moja miongoni mwa kazi tunayokwenda kuifanya ni kwenda kutatua changamoto ya uingiaji wa maji ya bahari sambamba na kujenga kuta za aina zote zinazohusika katika maeneo hayo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa, fedha zile zitakapokuwa tayari, tutakwenda kujenga maeneo mengi lakini Nungwi tutakwenda kuipa kipaumbele. Ninakushukuru.

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Supplementary Question 4

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Tumepata maelezo mazuri jinsi Serikali itakavyoshughulikia maji kuongezeka katika fukwe za Bahari, lakini hali hii ya kujaa maji ipo pia katika maziwa yetu ambayo kuna sehemu nyingine miji pia imezama kabisa. Je, Serikali imejipanga vipi kufanya mkakati wa utafiti kwa jinsi itavyodhibiti maji yanavyojaa kwenye maziwa yetu na namna gani tuta-save maji haya kufanyia kazi nyingine badala ya kuzamisha miji yetu iliyopo katika maziwa?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba mara nyingi watu wamekuwa wakilia na kilio cha maji ya bahari kuingia katika makazi lakini ni kweli utafiti umeonyesha kwamba hata maji ya baadhi ya maziwa na mito mingine kina chake kinakuwa kikubwa na yanaingia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu jibu lipo pale pale kama tulivyoeleza katika jibu la msingi kwamba tumeanza kufanya utafiti kwa sababu hatuwezi kujenga ukuta kabla ya kufanya utafiti kujua aina gani ya ukuta unaotakiwa?

Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, tunaendelea kutafuta fedha na zitakapopatikana, nimwambie Mheshimiwa Asha na Waheshimiwa wote kwamba tunakwenda kujenga kuta kwenye maeneo yote yenye changamoto.

Name

Abdul Yussuf Maalim

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Amani

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Supplementary Question 5

MHE. ABDUL YUSSUF MAALIM: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali. Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu ya mazingira hasa kwa maeneo ya bahari ambayo yanatumiwa na masuala ya Uchumi wa Bluu?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba kuna baadhi ya maeneo yameathirika kutokana na shughuli za Uchumi wa Bluu ambazo zinaendelea. Kama unavyofahamu kwamba Uchumi wa Bluu ni uvuvi, lakini vilevile masuala ya ulimaji wa mwani, masuala ya harakati za utafiti kwa ajili ya ugunduzi wa mafuta na gesi na mambo kama hayo. Kwa hiyo, shughuli hizi zimekuwa zikiharibu mazingira kwa kiasi fulani.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tumechukua hatua mbalimbali zikiwemo za kuendelea kutoa elimu kwa wananchi, kwanza namna ya kufanya shughuli za uvuvi ambazo zinazingatia sheria. Pia, tumekuwa tukiwaambia wananchi kwamba sababu nyingine inayoathiri ni sababu kubwa ya watu kukata mikoko ama miti iliyo pembezoni mwa bahari.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hili tumeendelea kuwaelimisha wananchi kuwaambia kwamba pamoja na shughuli hizi zinazoendelea za Uchumi wa Bluu za uvuvi na mambo mengine, lakini miti iendelee kupandwa kwa sababu miti ndiyo uhai wa bahari. Kikubwa tumehimiza watu masuala ya usafishaji wa fukwe na mambo mengine kama hayo ili shughuli za Uchumi wa Bluu ziendelee pia usafi, na sheria ya mazingira vizingatiwe.