Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Enviroment Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 536 2025-06-09

Name

Ally Mohamed Kassinge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kusini

Primary Question

MHE. FRANCIS K. NDULANE K.n.y. MHE. ALLY M. KASSINGE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje ili kuzuia maji ya Bahari yanayoathiri Wananchi?

Name

Khamis Hamza Khamis

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Uzini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu: -¬
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kuchukua hatua mbalimbali za kukabiliana na athari kubwa ya mabadiliko ya tabianchi zinazochangia kuongezeka kwa kina cha Bahari na kuathiri fukwe mbalimbali ikiwemo eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua hizo ni pamoja na kuendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa fukwe zote katika Ukanda wa Pwani ikiwemo Kilwa Kivinje na kuendelea kutenga fedha na kutafuta fedha kupitia Mifuko ya Usimamizi wa Mazingira na Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi ikiwemo, Mfuko wa Kuhimili Mabadiliko ya Tabianchi (Adaptation Fund), GEF na GCF na Washirika wa Maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa muktadha huo, shughuli za ujenzi wa ukuta eneo la Pwani ya Mji wa Kilwa Kivinje zitaanza kutekelezwa baada ya fedha kupatikana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda kuchukua fursa hii kuhimiza uongozi na wananchi wa Kilwa Kivinje kuendelea kuongeza jitihada za kutunza na kuhifadhi mazingira ya maeneo ya ufukwe na kudhibiti shughuli zisizo endelevu za kibinadamu na kuongeza jitihada za uhifadhi wa mazingira, upandaji wa miti kama ilivyobainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru.