Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:- Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha inawawezesha kiuchumi Watu wenye Ulemavu.

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipatia nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa, Serikali inaonesha imewezesha maeneo mbalimbali ya kiuchumi kwa watu wenye ulemavu, lakini bado kuna watu wenye ulemavu wengi sana hawaelewi wapi waende wakapate fursa hizo. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuongeza elimu kwa watu wenye ulemavu ili waelewe fursa ambazo wanapewa na Serikali?

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imendelea kufanya kazi kubwa sana ya kutoa elimu, pia kuhamasisha na kuwaunganisha watu wenye ulemavu. Itakumbukwa mwaka 2022 Mheshimiwa Rais alikutana na watu wenye ulemavu pale Chamwino - Ikulu na akawasikiliza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya mambo ambayo ni makubwa yalifanyika, kwanza ni kuimarisha Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu ambapo aliwanunulia mpaka kiwanja kwa ajili ya kujenga makao makuu yao kama chombo cha kuwasaidia kupata taarifa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua ya pili Mheshimiwa Rais pia kwa maagizo yake mahsusi alitaka kuwepo kwa uwezesho wa ruzuku kupitia Mfuko wa Watu Wenye Ulemavu hasa kupitia SHIVYAWATA zaidi ya shilingi bilioni moja inatengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tatu, kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu tumeendelea kukutana na makundi mbalimbali ya watu wenye ulemavu na kutoa elimu kupitia vyombo vya habari, redio, magazeti pia kukutana nao katika makundi mbalimbali hasa kwenye sekta ambazo wapo watu wenye ulemavu. Kwenye sekta ya sanaa tunao Jumuiya Band na bendi nyingine za watu wenye ulemavu ambapo tunawasaidia pia kama Serikali kuweza kujitangaza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwenye michezo pia Tembo Warriors ambayo ni Timu ya Watu Wenye Ulemavu ambapo pia tumeendelea kuonesha kwamba katika hayo maeneo tunawatambua. Kwenye kilimo wapo, wanapewa maeneo kama mpango uliopo kwenye programu za kilimo, madini hata kwenye eneo lingine la watu wenye ulemavu kwenye utoaji wa elimu wameendelea kufikiwa, kwa maana ya kuhamasishwa kwenda kwenye vyuo vya ufundi na marekebisho ya watu wenye ulemavu ambapo kuna vyuo zaidi ya saba ambavyo vilikuwa havifanyi kazi, Mheshimiwa Rais alitoa zaidi ya shilingi bilioni 3.6 kuvifufua na vimeshaanza kufanya kazi kwenye maeneo mbalimbali, pia tunajenga vyuo vingine vipya.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hivyo, ujumuishwaji wa watu wenye ulemavu na utoaji wa elimu unagusa kila sekta ambapo watu wenye ulemavu wapo na Serikali tumeendelea kufanya hivyo. Ninaomba pia Waheshimiwa Wabunge kwenye maeneo yao waendelee kuiona ofisi hii. Tupo wazi kwa ajili ya kuendelea kusaidia watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na mashirika yote yanayojihusisha na watu wenye ulemavu. Ahsante.