Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 42 Youth, Disabled, Labor and Employment Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana na Wenye Ulemavu 533 2025-06-09

Name

Minza Simon Mjika

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y. MHE. MINZA S. MJIKA aliuliza:-

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha inawawezesha kiuchumi Watu wenye Ulemavu.

Name

Paschal Katambi Patrobas

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Shinyanga Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU (MHE. PASCAL P. KATAMBI) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Minza Simon Mjika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kuwawezesha kiuchumi Watu wenye Ulemavu, Serikali imeendelea kufanya yafuatayo: -

(1) Kutoa Mikopo ya 10% isiyokuwa na riba inayotokana na mapato ya ndani ya Halmashauri kwa ajili ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu, ambapo watu wote wenye ulemavu wametengewa asilimia mbili;

(2) Utekelezaji wa takwa la Sheria ya Ununuzi wa Umma, Sura 440 la kutenga 30% ya zabuni za umma kwa ajili ya wanawake, vijana, wazee na watu wenye Ulemavu;

(3) Utekelezaji wa mipango ya maendeleo endelevu ya watu wenye ulemavu na ile ya kibajeti ikiwemo fungu maalum kwa wenye ulemavu;

(4) Kuwapatia elimu itakayowawezesha kushiriki katika shughuli jumuishi za kiuchumi; na

(5) Utekelezaji wa miongozo mbalimbali ukiwemo ule wa matumizi ya teknolojia saidizi ili kuwawezesha nao kushiriki katika shughuli za kiuchumi.