Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Shabani Omari Shekilindi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lushoto
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Gari jipya la Wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa kuwa lililopo limechakaa?
Supplementary Question 1
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI: Mheshimiwa Spika, ninakushuku na nina maswali mawili ya nyongeza. Tuna vituo vya afya zaidi ya vitatu katika Jimbo la Lushoto, lakini chenye gari la wagonjwa ni kituo kimoja tu cha Mlola: -
Je, Serikali haioni kuwa kuna haja ya kuongeza bajeti ya kuwa na magari mawili ili kurahisisha usafiri kwa wagonjwa wetu?
Mheshimiwa Spika, swali la pili, wananchi wa Lushoto wamejenga zahanati mbili, Kata ya Kilole ambayo ni Mbeleyi na Kata ya Makanya ambayo ni Mdando. Hata hivyo, zahanati zile wamejenga kwa nguvu zao na hazijaisha: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza fedha kwa ajili ya kumalizia zahanati zile ili kuondoa usumbufu kwa wanaosafiri kufuata huduma za afya?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kama ambavyo katika mwaka wa fedha 2023/2024 Serikali ilipeleka magari mapya mawili ya wagonjwa katika Halmashauri ya Lushoto, tunafahamu kwamba vipo vitu vya afya ambavyo vinahitaji magari ya wagonjwa, na tunafahamu kwamba safari ni hatua; tutaendelea kununua magari haya kwa awamu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tayari magari mawili yamekwenda; na nimhakikishie kwamba, vituo vingine vya afya vitaendelea kupewa magari ya wagonjwa kwa kadri ambavyo tutakuwa tumeweka kwenye bajeti.
Mheshimiwa Spika, kwa swali la pili, kuhusu vituo vya afya katika kata hiyo, Kituo cha Afya Mbeleyi na Mdando. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Ofisi ya Rais - TAMISEMI tulikwishafanya tathmini na kuandaa mpango mkakati wa utekelezaji wa ujenzi na ukamilishaji wa vituo vya afya katika kata zote za kimkakati, zikiwemo kata hizo mbili ambapo kuna Kituo cha Afya cha Mdando na Mbeleyi.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Shekilindi kwamba Serikali itaendelea kupeleka fedha na tutahakikisha kwamba tunapeleka fedha kwa ajili ya vituo hivyo vya afya.
Name
Abubakar Damian Asenga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilombero
Primary Question
MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka Gari jipya la Wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa kuwa lililopo limechakaa?
Supplementary Question 2
MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Kata ya Msola Station Kipo umbali wa kilometa 22 mpaka Mkamba: -
Je, ni lini Serikali itapeleka gari la wagonjwa (ambulance) katika Kituo cha Afya cha Kata ya Msola Station?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Asenga, kwa sababu alikwishaleta hoja hiyo na tunatambua kuwa kituo kile cha afya kinahudumia wananchi wengi, lakini pia kiko umbali mkubwa kutoka kituo cha afya chenye gari la wagonjwa; tayari tumekiweka kwenye mpango wa vituo vya afya ambavyo vitapelekewa magari ya wagonjwa hivi karibuni.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved