Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Regional Administration and Local Government Authorities Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 319 2025-05-15

Name

Shabani Omari Shekilindi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lushoto

Primary Question

MHE. SHABANI O. SHEKILINDI aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka Gari jipya la Wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto kwa kuwa lililopo limechakaa?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto mwaka 2023/2024 imepokea magari mawili ya kubebea wagonjwa na kupelekwa katika Vituo vya Afya vya Mlola na Mtae. Kwa sasa Hospitali ya Wilaya ya Lushoto inatumia gari la kubebea wagonjwa kutoka kwenye Kituo cha Afya Mlola wakati taratibu za matengezo ya gari la hospitali ya wilaya zikiendelea.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini; na Hospitali ya Wilaya ya Lushoto itapelekewa gari.