Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Abdi Hija Mkasha
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Micheweni
Primary Question
MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha Kituo cha TEHAMA kilichopo Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 1
MHE. ABDI HIJA MKASHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, lakini nina maswali mawili ya nyongeza (a) na (b) kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa Serikali imekiri kuwepo kwa changamoto katika kituo kile; je, ni lini itaharakisha kwenda kufanya tathmini hiyo? (Makofi)
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili, kwa kuwa katika kituo kile kuna vijana ambao wanajitolea, je, Serikali ipo tayari kuwafanyia mpango angalau wa kupata posho ya kuweza kujikimu? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwanza, ninampongeza sana Mheshimiwa Abdi Mkasha kwa kufuatilia maslahi ya vijana ambao wako pale tayari wanafanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu kwenye jibu langu la msingi, tayari sisi kama Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kwa Tanzania Bara tulishafanya sehemu yetu kupitia UCSAF na tayari tumeshakabidhi kwenye Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara hii ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi. Hivyo, ninapenda tu kukwambia kwa sababu tunafanya kwa ushirikiano basi nitawasiliana na wewe na kuona namna njema ya kukukabidhi kwa wenzetu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ili waweze kufanya haya wote mawili; kuharakisha katika maboresho, lakini vilevile kuangalia maslahi ya vijana. (Makofi)
Name
Omar Issa Kombo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wingwi
Primary Question
MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha Kituo cha TEHAMA kilichopo Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 2
MHE. OMAR ISSA KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwa kuwa kituo hiki wamekuwepo vijana na wamejitolea kwa muda mrefu na kwa kuongeza kasi ya kuwapatia vijana mafunzo na kuzingatia maendeleo makubwa ya teknolojia, je, Serikali ya SMZ pamoja na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haioni haja ya kukaa pamoja kuwapatia ajira za moja kwa moja hawa vijana ili kuwapa moyo wa kufanya kazi kwa bidii zaidi? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante na ninashukuru sana kwa swali zuri ambalo linaendelea kukazia maslahi ya vijana kuona sasa wanapata ajira. Tunafahamu taratibu za ajira za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zilivyo na sisi kama Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuna Sekretarieti ya Ajira na tuna Wizara ya Utumishi, lakini haya yote kwa sababu tayari wako ndani, vigezo na masharti vitazingatiwa kuona namna gani wanaweza kupatiwa ajira. (Makofi)
Name
Yahya Ally Mhata
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyumbu
Primary Question
MHE. ABDI HIJA MKASHA aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha Kituo cha TEHAMA kilichopo Wilaya ya Micheweni?
Supplementary Question 3
MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, kwenye Tarafa ya Nakopi, Kata ya Napacho, Kampuni ya Minara Tanzania ilipewa kazi ya kusimika minara katika eneo hilo, jambo ambalo sasa ni mwaka mmoja huo mnara haujasimikwa. Changamoto kubwa ni mawasiliano ya kufika katika eneo ambalo mnara unatakiwa kujengwa.
Je, Serikali iko tayari kuisaidia hii Kampuni ya Minara Tanzania wakatengeneza miundombinu ya barabara ili waweze kufika katika eneo ambalo limekusudiwa kujengwa mnara huo? (Makofi)
Name
Kundo Andrea Mathew
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bariadi Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Yahya kuhusu barabara ya kufika katika maeneo ya ujenzi wa minara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama Wizara tayari tumeshafanya mawasiliano na wenzetu wa TAMISEMI kuona TARURA inaweza kuingilia kati na kuona namna njema ya kusaidiana na hawa watoa huduma ili waweze kutengenezewa barabara.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pia wakati mwingine wananchi wanaweza wakatoa nguvu kazi kama inawezekana kulingana na jiografia ili kuona minara hii inajengwa na maeneo hayo yanaweza kupitika.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved