Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:- Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Mheshimiwa Naibu Waziri ninakupongeza sana kwa hatua zako za kufuatilia ujenzi wa Chuo Kikuu cha Chato ahsante sana Mheshimiwa, Mungu akubariki sana.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda nitoe shukrani nyingi kwa Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa fedha shilingi milioni 900 kuanza ujenzi wa Chuo Kikuu hiki cha Kasagara Mjini Chato. Mheshimiwa Naibu Waziri tufikishie shukrani nyingi sana za Wananchi wa Chato kwa ujenzi wa chuo kikuu kwa Mheshimiwa Rais wetu. Nina maswali mawili ya nyongeza. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; ni kweli ujenzi ungeanza mwaka 2021, lakini kwa sababu za kimkataba, mkandarasi ameshindwa kuendelea na ujenzi sasa swali langu la kwanza, ni lini Serikali itapata mkandarasi huyo mpya na kuanza ujenzi? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; ninapenda nimwulize Mheshimiwa Naibu Waziri na kwa sababu yupo tayari kufuatana na mimi, ni lini tutaongozana wote kwenda kuwaambia Wananchi wa Chato kuhusu kukamilisha ujenzi wa chuo kikuu na hasa ndani ya kipindi hiki kabla ya mwisho wa Bunge hili? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Dkt. Kalemani, Mbunge wa Chato, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyokwishaeleza kwenye majibu ya swali la msingi kwamba, ujenzi huu ulianza toka mwaka 2021 na umesimama au ulisimama kutokana na changamoto hizo za kimkataba. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge tarehe 27 Januari, 2025 mkandarasi pamoja na Chuo kikuu cha Dar es Salaam pamoja na consultant tuliwaita Wizarani kwa lengo la kujua maendeleo na changamoto za mradi huu. Baada ya kikao kile ndipo ilipobainika kwamba warudi sasa waende wakakae wafanye settlement ya mkataba ule.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna mambo yalikuwa ni lazima yafanyike ambayo la kwanza, ikafanyike conditional survey; pili, ifanyike evaluation ya kazi iliyofanyika mpaka pale tulipofikia pamoja na remeasurement; tatu, iandaliwe final account; lakini la mwisho, kabisa yalipwe yale malipo ya mwisho kulingana na kazi pale ilipofikia na baada ya hapo sasa ndipo tunaweza tukafanya engagement ya kutangaza ile kazi kwa ajili ya kumpata mkandarasi mwingine.

Mheshimiwa Mwenyekiti, tupo katika hatua za mwisho michakato hii yote niliyoitaja tayari imekamilika na ni matarajio yetu kwamba itakapofika mwezi Juni utaratibu wa kutangaza kazi hii na kumpata mkandarasi mwingine kwa ajili kuanza kazi hii itakapofika mwaka ujao wa fedha tuwe tumeanza rasmi. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Wananchi wa Chato jambo hili Mheshimiwa Rais lakini Serikali hii ya Awamu ya Sita inasimamia vizuri.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo hiki cha chuo kikuu ni muhimu sana Waheshimiwa Wabunge kwa sababu tumeshajenga tayari kule Zanzabar eneo la Buyu, lakini tumejenga Kunduchi kituo kama hiki sasa hivi vilikuwa vinahudumia maeneo yale ya Bahari ya Hindi. Kwa upande wa maji baridi tulikuwa hatuna kituo chochote, kwa hiyo, kituo hiki ni muhimu na Serikali inaona umuhimu wa mradi huu kwa hiyo utaendelea kama ulivyopangwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili, kwamba ni lini? Ninaomba Mheshimiwa Mbunge aridhie kwa sababu wiki ijayo tuna bajeti ya Wizara ya Elimu mara baada tu bajeti yetu kupitishwa hapa tutapanga siku katika wikiendi zitakazofuata tuweze kwenda kule Chato kwenda kuwaambia wananchi nini mkakati wa Serikali juu ya jambo hili. Ninakushukuru sana.

Name

Francis Kumba Ndulane

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilwa Kaskazini

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:- Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. FRANCIS K. NDULANE: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Chuo cha VETA Wilayani Kilwa ili elimu ya ufundi stadi iweze kutolewa kwa vijana wetu? (Makofi)

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali dogo la Mheshimiwa Ndulane, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimwondoe hofu Mheshimiwa Ndulane na Waheshimiwa Wabunge wote ambao tunajenga vyuo 64 vya wilaya vile vya VETA na chuo kimoja cha mkoa katika Mkoa wa Songwe. Maendeleo ya miradi hii yote ni mizuri tayari tumeshapata fedha kwa ajili ya umaliziaji. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge target yetu au malengo yetu ifikapo mwezi Agosti mwaka huu vyuo hivi vyote viwe vimekamilika katika maeneo yote yale 64 na kile kimoja cha mkoa ili mwezi wa kumi zile course fupi ziweze kutolewa. Ninakushukuru sana.

Name

Abubakar Damian Asenga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilombero

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:- Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Supplementary Question 3

MHE. ABUBAKARI D. ASENGA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kutumia nafasi hii kutoa pole kwa wananchi wangu ambao wamekumbwa na mafuriko, jana nilikuwa Bungeni. Sasa kwa kuwa Serikali ina mpango mkakati mkubwa wa maendeleo ya kilimo katika Bonde la Kilombero hasa katika kilimo cha mpunga na miwa ya sukari na tuna chuo chetu cha Kilombero Agriculture Training and Research Institute (KATRIN) kina ekari karibu 400 na Serikali imepeleka pesa nyingi sana pale kwa kujenga mabweni na baadhi ya majengo kwa ajili ya training hiyo. Je, Wizara ya Elimu ina mpango gani wa kuhakikisha KATRIN sasa inakuwa tawi la Chuo Kikuu cha Kilimo?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nikijibu swali dogo la Mheshimiwa Asenga, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninampongeza sana Mheshimiwa Asenga kwa kufuatilia jambo hili. Ninakumbuka alishawahi kuja Wizarani kwa ajili ya kufuatilia jambo hili. Kwa hiyo, nikupongeze na kuahidi tu bado Serikali kupitia Wizara ya Elimu, tunalifanyia kazi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala haya ya kuanzisha matawi mbalimbali ya vyuo vikuu, ni masuala ambayo yanaendelea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Asenga pamoja na Wabunge wote, Serikali hii ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Awamu ya Sita tayari hivi sasa tunavyozungumza tunajenga Kampasi ya Chuo Kikuu hiki cha Kilimo kule Mpimbwe kwa Mheshimiwa Pinda. Kazi inaendelea kuhakikisha tawi lile linaimarika na limeshaanza kutoa huduma na kule Tunduru nako vilevile tunafanya kazi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kule Butiama tuna chuo kingine tunaanzisha ambacho kitakuwa cha kilimo, lakini ukienda Lindi kupitia chuo chetu cha Dar es Salaam tuna tawi ambalo tunaanzisha pale. Ninaomba nichukue tu ushauri huu wa Mheshimiwa Asenga ili tuhakikishe kwamba tunaingiza kwenye tathmini yetu ya Serikali tukishirikiana na wenzetu wa Wizara ya Kilimo ili kuona namna bora ya kufanya na eneo hili alilolitaja kama linaweza likawa ni kituo au branch ya Chuo chetu cha Kilimo cha Sokoine. Ninakushukuru sana.

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:- Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Supplementary Question 4

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Ushetu ni kati ya jimbo ambalo liliahidiwa kujengewa shule ya ufundi mwaka juzi lakini haikutekelezwa, mwaka jana pia nikaahidiwa, lakini haikutekelezwa. Sasa ninataka nijue commitment ya Serikali. Je, mwaka huu Serikali itaenda kunijengea shule yangu ya ufundi katika Jimbo la Ushetu?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru na ninamshukuru Mheshimiwa Mbunge wa Ushetu. Mheshimiwa Mbunge tayari alishakuja Wizarani chungu nzima, tumekuwa tukijadili hapa Bungeni mara kadhaa juu ya ujenzi wa shule yake ya ufundi katika jimbo lake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwondoe hofu, katika mgao uliopita wa awamu ya kwanza, zile shilingi milioni 528 bahati mbaya Jimbo la Ushetu halikuwa allocated, lakini tuna mgao wa awamu ya pili kwa sababu ujenzi ule wa shule zote za ufundi zaidi ya shule 103 unajengwa kwa awamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimhakikishie tu katika awamu hii ya pili ambayo tunatarajia kati ya mwezi huu au mwezi Juni, awamu ya pili ya zile fedha shilingi milioni 528 zitakuwa zimetoka na Jimbo la Ushetu litakuwemo kwa maana ya kuanza ujenzi wa shule hiyo ya ufundi katika jimbo lake.

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:- Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kuniona. Kuna hivi vyuo vishiriki vinajengwa vingi sasa kila mahali, branches nyingi za vyuo vikuu. Je, Serikali sasa mko tayari kutoa jedwali litakaloonesha hivi vyuo vyote vipya vinavyojengwa vimefikia asilimia ngapi? Ahsante.

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nikijibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Ntara, kuhusiana na maendeleo ya kampasi zetu za vyuo vikuu katika mikoa zaidi ya 14 ya Tanzania Bara pamoja na Tanzania Zanzibar na yeye lengo lake ni kutaka kujua tu project report kwa maana ya kutengeneza jedwali la asilimia mahali ilipofikia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba tu Mheshimiwa Dkt. Thea aridhie jedwali hili lipo na kama atalihitaji basi tunaweza tukawasiliana ili tuweze kuwasilisha kwa sababu kila mwezi taarifa hizi zimekuwa zinakuja Wizarani, lakini na sisi tumekuwa tunaziwasilisha kule Benki ya Dunia kwa maana ya kupata mrejesho na kujua ni namna gani fedha zitaendelea kutolewa na Benki ya Dunia. Ninakushukuru sana.