Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 224 2025-05-05

Name

Dr. Medard Matogolo Kalemani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chato

Primary Question

MHE. DKT. MEDARD M. KALEMANI aliuliza:-

Je, lini Ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam cha masuala ya samaki eneo la Kasagara - Chato ulioanza 2021 utakamilika?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Kasagara – Chato ulipaswa kuanza mwaka 2021 na kukamilika mwezi Mei, 2023. Ujenzi huo haujakamilika kutokana na changamoto za mkandarasi kushindwa kuendelea na ujenzi kwa muda mrefu hivyo kupelekea Serikali kuanza mchakato wa kusitisha mkataba wa utekelezaji wake. Taratibu za kufunga mkataba huo kisheria zinaendelea na mara zitakapokamilika Serikali itaanza mchakato wa kumtafuta mkandarasi mwingine ili kuendelea na ujenzi. Ninakushukuru sana.