Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Dr. Alice Karungi Kaijage

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali na tunaipongeza kwa juhudi ambazo imefanya kutatua tatizo hili katika Wilaya ya Rufiji Mheshimiwa Subira ana maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la kwanza; hii Kata ya Ngarambe na Mwaseni, shida hii imekuwa kubwa sana; wameweza kuweka nyuki kwa ajili ya kuzuia hawa tembo. Sasa kwa vile hili suala la kulipa fidia limekuwa ni la kusumbua kidogo na inagharimu sana Serikali. Je, hawaoni sasa kuna haja ya kuwawezesha wananchi wa kata hizi mbili ili waweze kuwa na shughuli mbadala kama ya ufugaji wa nyuki? Ahsante.

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; shida kama hii ipo katika Kata za Wilaya ya Bagamoyo ambayo ni Kata ya Mkange pamoja na Kiwangwa; je, Serikali ina mpango gani pia kuwafikia wananchi wa kata hizi za Wilaya ya Bagamoyo? Ahsante.

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nimesema kwenye jibu la msingi tumejitahidi kuendana na kutoa mikakati mbalimbali ambayo tumekwenda nayo kwa ajili ya kunusuru wananchi wa eneo hili na mojawapo ni kuanza kutumia mizinga ya nyuki kwa ajili ya kuzuia uharibifu unaoletwa na wanyama hawa (tembo). Ni imani yetu kwamba mizinga hii itatumika vilevile kama sehemu ya shughuli ya kiuchumi kwa wananchi wetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika eneo la pili alilolizungumzia kuhusu changamoto kule Bagamoyo, ni kweli tuna changamoto katika eneo la Bagamoyo tunapopakana na Hifadhi ya Saadan, kuna makundi makubwa yanayoenda kwenye maeneo ya kilimo cha miwa na tumeanza kuchukua hatua kwa kushirikiana na wenye mashamba yale kuona jinsi ambavyo tunaweza kuona jinsi ambavyo tunaweza kuanza kulinda maeneo yale kwa kutumia uzio wa umeme. Tupo katika hatua ya juu kufikia kupata suluhisho hilo lakini vilevile, tumepeleka mabomu baridi kule, na hivi karibuni tayari tuna mpango wa kupeleka ndege nyuki ili kuwanusuru wananchi. Kwa hiyo, ninaamini ndani ya kipindi kifupi suluhu ya changamoto hii itapatikana.

Name

Jeremiah Mrimi Amsabi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Serengeti

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 2

MHE. JEREMIAH M. AMSABI: Mheshimiwa Mwenyekiti, je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti wanyamapori waharibifu wanaotoka ndani ya hifadhi ya Taifa ya Serengeti pamoja na mapori ya akiba ya Ikorongo na Gurumeti na kuvamia vijiji vilivyopo Kata za Nata, Isenye, Nagusi, Mesocho, Sedeko na Mbalibali na kusababisha uharibifu mkubwa? Ahsante sana.

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mikakati ya kupambana na changamoto ya wanyama wakali na waharibifu ukanda ule wa Serengeti, Serikali imejiimarisha kwa kuongeza doria za udhibiti kwenye maeneo haya, lakini vilevile kuimaraisha vituo vyetu vya kudhibiti wanyamapori. Kama Mheshimiwa Mbunge anavyofahamu hivi karibuni tumeimarisha kituo chetu katika eneo lile lakini vilevile, kwa kushirikiana na wenzetu wa Frankfurt Zoological Society tumepeleka gari kwenye eneo hili. Ninaamini kwamba jitihada hizi sasa zitapunguza changamoto hii ambayo wananchi wa ukanda ule wamekuwa wakipambana nayo.

Name

Eng. Stella Martin Manyanya

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Nyasa

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 3

MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na kuikumbusha Wizara kuhusu kulipa kifuta machozi kwa familia tatu ya Lundo, Kingerikiti pamoja na Lipingu ambao wapendwa wao (ndugu zetu) walikamatwa na mamba katika Ziwa Nyasa na Mto Mbahwa. Je, kutokana na matukio hayo sasa kuwa ni mengi na mamba wanaonekana wengi wakizagaa zagaa kwenye Ziwa Nyasa ambalo tunatangaza utalii kwa kila hali, inakuwa tishio sasa kwa watalii. Lini Serikali itafanya maamuzi madhubuti ya kuwavuna mamba hao ikizingatiwa kwamba hata ngozi zao vilevile ni biashara kubwa? (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Mheshimiwa Mbunge aliwasiliana na mimi juu ya matukio haya matatu yaliyotokea ya mashambulizi ya mamba na tayari tumewaelekeza wataalamu wetu wa TAWA kupeleka timu kwenye eneo lile kwenda kufanya tathmini ya uhalali wa malipo yale, lakini vilevile kuweka mikakati ya kuwavuna mamba katika eneo lile. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira, jambo hili tunalifanyia kazi.

Name

Hassan Zidadu Kungu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduru Kaskazini

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 4

MHE. HASSAN Z. KUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, moja ya sababu ya tembo kuvamia makazi ya watu ni pamoja na wafugaji kwenda kufuga kwenye hifadhi za wanyamapori. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwahamisha ama kuwaondoa wafugali wanaofanya shughuli za ufugaji kwenye hifadhi ili kuondoa hii adha kubwa ya tembo kuvamia makazi ya watu? Ahsante.

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imechukua jitihada za makusudi kuhakikisha kwamba watu walioingiza mifugo kwenye maeneo ya hifadhi wanachukuliwa hatua. Serikali kwa kushirikiana na Serikali ya Mkoa imetenga maeneo kwa ajili ya wafugaji hao kuelekeza mifugo yao na tayari Serikali inafanya jitihada za kuhakikisha makundi haya ya ng’ombe yaliyopo katika hifadhi zetu yanatoka ili wafugaji aelekezwe kwenye maeneo yale. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge tuendelee kuwa na subira wakati kazi hii inaendelea kufanyika kwenye maeneo yale.

Name

Ritta Enespher Kabati

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 5

MHE. DKT. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, kumekuwa na tembo wengi sana katika Tarafa ya Mahenge katika Wilaya ya Kilolo wamekuwa wakifanya uharibifu mkubwa wa mazao na mali za watu na kuua watu, lakini kifuta machozi na fidia hailipwi kabisa. Je, Serikali inatoa tamko gani kwa wananchi ambao hawapati fidia hizo? (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza si kweli kwamba kifuta jasho na kifuta machozi hakilipwi kabisa. Serikali inafanya kazi kubwa ya kufanya tathmini ya pale inapopata madai haya, kwenda kuyafanyia uchambuzi ili wananchi waweze kulipwa na katika kufanya hilo mwezi wa pili tuliwaita Maafisa Wanyamapori wote wa wilaya zote nchini kuja kuwapa semina na maelekezo ya jinsi ya kutumia mfumo wa kidigiti katika kukusanya takwimu za matukio katika maeneo yao na kuweza kuyaleta kwa haraka. Pale tunapoona kwamba kuna ucheleweshaji wa malipo ni kwa sababu wataalam wetu katika ngazi ya halmashauri wamekuwa wakichelewesha kuleta madai haya Serikalini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inafanya kazi kubwa ya kulipa madai haya tunapoyapata kwa wakati. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge kama anayo madai ya wananchi wake baada ya kikao hiki cha leo tuwasiliane aweze kunipatia ili tuweze kuyafanyia kazi.

Name

Yahya Ally Mhata

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyumbu

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 6

MHE. YAHYA A. MHATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii. Leo hii tarehe tano mwezi Mei ndani ya Jimbo langu la Nanyumbu tunamzika ndugu yetu Hassan Napicha ambaye ameuawa na tembo sehemu ya Chinanyila, kwenye Kijiji cha Chinyanyila. Changamoto kubwa iliyopo ndani ya Jimbo langu ni kuongezeka zaidi kwa wanyama hawa (tembo) na wilaya nzima haina ndege nyuki ya kuwafukuza tembo hawa. Je, Serikali ipo tayari kutoa kauli leo, ni lini tutapatiwa ndege nyuki ambayo ikawa stesheni pale wilayani ili iweze kukabiliana na wanyama hawa waharibifu? (Makofi)

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mhata, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kwa naiba ya Serikali tunaomba kutoa pole kwa ndugu zetu ambao wamepoteza mpendwa wao kutokana na kadhia hii ya tembo katika siku hii ya leo kwenye eneo lile. Pili, Serikali imepeleka ndege nyuki tano katika Ukanda wa Kusini pamoja na maeneo ya Nanyumbu na maeneo mengine. Ninaomba wataalam wetu wafanye haraka kuhakikisha kwamba kunakuwa na operation maalum katika eneo lile la Nanyumbu ili kukabiliana na wanyama hawa (tembo).

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 7

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kuwa uharibifu wa wanyama katika maeneo ya Vijiji vya Unyali, Kihumbu, Mariwanda, Sarakwa, Mugeta, Kyandege na Tingirima ni mkubwa sana na kwa kuwa Kampuni ya VIP imeonesha nia ya kuweka fence ya waya kwa kulinda tembo. Ni nini kinachosababisha Serikali isii-support Kampuni ya VIP ili kuweka fensi kwenye maeneo ya uharibifu? Ninakushukuru.

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Getere, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mpaka unaposikia kwamba kampuni fulani inataka kuweka fence ni kwamba tayari imekwishakuwa na mawasiliano na kupata ushirikiano kutoka Serikalini kwa ajili ya kufanya jambo hilo, vinginevyo wasingekuwa hata na ndoto ya kufanya jambo hilo. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inashirikiana na taasisi hizi lakini yapo mambo ya kimsingi lazima yafanyike kuhakikisha kwamba hilo la kuweka fence linatokea. Ninamwomba Mheshimiwa Mbunge awe na subira wakati taratibu hizi za kikanuni zinafanyiwa kazi ili jambo hilo liweze kutokea.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:- Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?

Supplementary Question 8

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Mwenyekiti, mimi mwenyewe nimekuwa nikifuatilia malipo ya fidia ya wananchi wangu katika jimbo langu sasa hivi ni takribani mwaka na jambo hili Mheshimiwa Naibu Waziri analifahamu kwa sababu nimekuwa nikienda kwake mara kwa mara kufuatilia jambo hili. Tumeambiwa turekebishe pale, tukarekebisha, rekebisha hapa tumerekebisha, lakini mpaka sasa hivi hawajalipwa. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri anasemaje kuhusiana na jambo hili, ni lini atawasaidia watu hawa kwa sababu miongoni mwao wanahitaji matibabu?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali moja la nyongeza la Mheshimiwa Mchungahela, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, nimshukuru kwa kukiri kwamba taarifa ambazo tumekuwa tukizipokea kutoka kwenye wilaya yake ni taarifa ambazo si sahihi, ni taarifa ambazo zimekuwa na mapungufu makubwa. Wizara kwa kushirikiana na wataalamu wale, tumekuwa tukifanya mawasiliano ya karibu kuhakikisha kwamba taarifa zile zinakuwa na viambatisho vyote vinavyostahili na vitakavyotuwezesha kufanya malipo. Tumepata taarifa zile tupo katika hatua ya kukamilisha jambo hili. Ninaomba kama ambavyo amekuwa na ushirikiano wa karibu kwenye jambo hili, tuendelee kushirikiana ili tukamilishe kuwalipa wananchi wale.