Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 15 | Sitting 17 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 223 | 2025-05-05 |
Name
Subira Khamis Mgalu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. DKT. ALICE K. KAIJAGE K.n.y. MHE. SUBIRA K. MGALU aliuliza:-
Je, kuna mpango gani kuwasadia wananchi wa Kata za Ngarambe na Mwaseni - Rufiji kukabiliana na wanyama waharibifu hasa Tembo?
Name
Dunstan Luka Kitandula
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mkinga
Answer
NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na changamoto ya wanyamapori wakali na waharibifu, kuanzia mwezi Julai, 2024 hadi mwezi Machi, 2025 Serikali imechukua hatua mbalimbali ikiwemo; kufanya doria za kudhibiti matukio 293 ya wanyamapori wakali na waharibifu. Vilevile, kuendelea kuimarisha kituo cha kudumu cha udhibiti wa wanyamapori wakali na waharibifu kilichopo katika Kata ya Ngarambe. Pia kuvuna mamba 15 na viboko wanne katika Mto Rufiji na maeneo yanayopakana na mto huo; kununua ndege nyuki moja inayotumiwa na Askari wa Pori la Akiba Selous.
Mheshimiwa Mwenyekiti, hatua nyingine ni kutumia Askari wa mkataba 20 waliohitimu Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza; kutoa mizinga ya nyuki 100 katika Kijiji cha Ngarambe Kitongoji cha Ngarambe Magharibi ambayo inatumika kuzuia tembo kuingia kwenye mashamba ya wananchi; na kutoa elimu ya uhifadhi na mbinu za namna ya kuepuka madhara ya wanyamapori wakali na waharibifu kwa wananchi 1,165 wa Vijiji vya Ngarambe, Tapika na Namakono katika Kata ya Ngarambe pamoja na Vijiji vya Mibuyu saba na Mtanza vilivyopo katika Kata ya Mwaseni.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved