Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti maudhui yasiyo na maadili katika mitandao ya kijamii kwa maslahi ya afya ya akili na watoto?
Supplementary Question 1
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; ni upi mkakati sasa wa kudumu wa kuweka vitu, kama censorship, ili kuzuia taarifa na maudhui yasiyo na maadili kusambaa katika Jamii ya Watanzania?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Serikali imejipanga vipi pia, kuzuia tamaduni na zile ngoma ambazo zinachezwa bila nidhamu, ikiwemo kucheza uchi, akinamama au wanaume wakiwa wanacheza wakiwa kwenye sherehe ambazo zinaadhimishwa katika Taifa letu. Ni upi mkakati wa Serikali kuzuia?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa maswali mazuri kutoka kwa Mheshimiwa Msambatavangu, kwa niaba ya Mheshimiwa Ng'wasi Kamani. Kwanza, Serikali imewekeza katika teknolojia, kupitia TCRA, Serikali imewekeza sana kwenye teknolojia, ikiwemo matumizi ya akili za bandia, ili kuhakikisha kwamba, inabaini na kuzuia ama kuondosha habari ambazo zimechapishwa na ziko kinyume na maadili ya Mtanzania kabla hazijawafikia walaji wengi zaidi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, la pili, Serikali kwa sasa ina ushirikiano mkubwa na kampuni kubwa zinazoendesha shughuli hizi duniani, kwa mfano, Google ama Meta, ambapo wanaendesha Facebook na Twitter, ili kuhakikisha habari ambazo hazina maadili, ambazo zimechapishwa, either zinazuiwa kuchapishwa ama zinaondolewa haraka. Halikadhalika, Serikali inaendelea kuboresha Sera na Sheria zinazotumika kuendesha masuala ya uchapishaji wa habari mtandao na inaendelea kuelimisha wananchi ili waendelee na wao kujilinda na masuala haya na kuhakikisha maadili hayakiukwi kwa kutumia machapisho haya yaliyoko mtandaoni.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo, kimsingi Serikali inafanya kila linalowezekana, ili kuhakikisha kwamba, uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kupata habari hautupeleki kwenye ukiukwaji mkubwa wa maadili na hivyo kuweza kulinda vizazi vyetu. Swali la pili, ilikuwa ni kuhusiana na ngoma zisizofaa. Haya mengineā¦
MWENYEKITI: Mavazi yanayovaliwa kwenye ngoma zisizofaa. Mavazi yanayovaliwa, ambayo siyo rasmi na mazuri.
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa. Hili moja kwa moja linakwenda kwenye uvunjifu wa Sheria za nchi na linatakiwa kuhudumiwa kwa namna hiyo. Kwa hivyo, kama kutakuwa na habari au mwonekano ambao haufai, masuala haya yanatakiwa kuripotiwa kwenye mamlaka zinazohusika yachukuliwe Sheria na yashugulikiwe kwa mujibu wa Sheria za Nchi. (Makofi)
Name
Issaay Zacharia Paulo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbulu Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti maudhui yasiyo na maadili katika mitandao ya kijamii kwa maslahi ya afya ya akili na watoto?
Supplementary Question 2
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina swali la nyongeza. Je, Serikali ina mkakati gani kwa kuwa hili kundi la watoto ndiyo litakaloathirika baadaye kutokana na maonyesho haya ambayo tunashindwa kuyazuia kwenye mitandao ya kijamii?
MWENYEKITI: Hajakuelewa vizuri, ninaomba uliweke kwa ufasaha.
MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri na mikakati mizuri ya Serikali, bado kuna tatizo kwa watoto wadogo kutokana na kufuatilia matangazo hayo kwenye vyombo vya televisheni hasa wanapokuwa wenyewe majumbani na pindi wanapokuwa kwenye ma-group. Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa elimu kwa wazazi ili kudhibiti hali hii, kwa sababu hili kundi ndilo litakaloathirika baadaye? (Makofi)
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kama ambavyo nilijibu wakati ninajibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Msambatavangu; moja ya mambo ambayo Serikali inafanya, pamoja na kuboresha sera na sheria zinazoendesha masuala haya, pia ni kutoa elimu kwa jamii nzima ili nayo iweze kujilinda, kujikinga na kuhakikisha kuwa vizazi vyetu havifikiwi na habari ambazo zina uvunjifu mkubwa wa kimaadili. Kwa hiyo ni rai yangu kwa wazazi na walezi kuhakikisha kwamba wanawakinga wanaowalea ama watoto wao kuhakikisha kwamba hawafikiwi na habari hizi na kupelekea mmomonyoko wa maadili.
Name
Felista Deogratius Njau
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti maudhui yasiyo na maadili katika mitandao ya kijamii kwa maslahi ya afya ya akili na watoto?
Supplementary Question 3
MHE. FELISTA D. NJAU: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali dogo la nyongeza. Mtandao wa TikTok ndio mtandao pendwa wa watoto wetu wanafunzi, lakini ndio mtandao unaoongoza kwa maudhui mabaya. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha kuwa wanadhibiti huu mtandao ili kunusuru watoto wetu waweze kukua kwa maadili ya Kitanzania?
Name
Hamis Mohamed Mwinjuma
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muheza
Answer
NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Mheshimiwa Mwenyekiti, upo ukinzano wa moja kwa moja upo kati ya ukuaji mkubwa wa teknolojia na uvunjifu wa maadili nchini. Serikali inachokifanya ni kuhakikisha kwamba wachapishaji wa habari na hii mitandao wanafuata sheria za nchi, ikiwemo ukaguzi wa mara kwa mara ambao unafanywa na TCRA, kwa sababu wote wanatakiwa kuwa wamesajiliwa na TCRA.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hivyo udhibiti unaendelea kufanyika, na pale ambapo tunaona kuna haja kabisa ya kuingia na kufuata mamlaka nyingine za kisheria ili kuhakikisha ya kwamba maadili hayaendelei kuvunjwa huwa tunafanya hivyo. Kuna ugumu wa kufanya hivi kwa sababu ya mkubwa wa teknolojia duniani, hata hivyo tunaendelea kurekebisha sera na sheria ambazo zinahudumia haya masuala.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved