Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo 220 2025-05-05

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU K.n.y. MHE. NG’WASI D. KAMANI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti maudhui yasiyo na maadili katika mitandao ya kijamii kwa maslahi ya afya ya akili na watoto?

Name

Hamis Mohamed Mwinjuma

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muheza

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeweka mikakati na inaendelea kuchukua hatua za kiudhibiti kuhusiana na maudhui yasiyo na maadili katika anga la mtandao hapa nchini, ikiwemo mitandao ya kijamii. Kufikia Tarehe 31 Machi, 2025 TCRA imeweza kubaini na kufungia tovuti, akaunti za mitandao ya kijamii, majukwaa, blogs na kadhalika, zipatazo 80,171 zilizokuwa zinachapisha maudhui yaliyo kinyume na maadili na yenye kuhatarisha afya ya akili na watoto. Zoezi hili ni endelevu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inaendelea kuendesha na kutoa mafunzo ya weledi kwa waandishi wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na wachapishaji wa maudhui mtandaoni. Mafunzo haya yanawajengea uwezo washiriki katika kutambua maudhui ghushi mitandaoni, uandaaji wa makala pamoja na ujenzi wa taswira ya nchi ili kuendelea kulinda utamaduni ulio salama kwa makuzi ya Jamii ya Watoto wa Kitanzania.