Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:- Je, Halmashauri ya Mpanda inanufaika vipi na mauzo ya mchanga wa marudio ya madini katika Kata ya Misunkomilo, Mpanda? (Makofi)

Supplementary Question 1

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo maswali mawili madogo ya nyongeza. Swali la kwanza; Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wamekuwa wakihifadhi mchanga wa madini (tailings) kwa muda mrefu. Kitu cha ajabu ni wao wameambiwa watapewa tozo tu ya huduma. Kwa nini wasipewe sehemu ya asilimia za mauzo ya mchanga huo? (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; awali, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda wamewahi kushiriki biashara ya kokoto katika eneo hilo hilo. Vigezo vilivyoiruhusu halmashauri kufanya biashara ya kokoto, kwa nini visitumike kwenye biashara hii ya tailings? Ninakushukuru.

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI K.n.y. WAZIRI WA MADINI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge na ninaomba niyajibu kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusuana na Halmashauri ya Mpanda kuwa sehemu ya mauzo na umiliki wa mauzo ya mchanga huu wa marudio na kuhusiana na swali lake la pili pia, kuhusiana na kushiriki katika biashara hii ya mchanga wa marudio, jambo hili linawezekana. Kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri, ninaomba niishauri Halmashauri ya Mpanda kufanya mazungumzo na mmiliki wa mchanga huo wa marudio, ili kuona uwezekano wa wao kuwa sehemu ya mauzo ya mchanga huo wa marudio.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Serikali, kupitia Wizara ya Madini, tutafurahi kushiriki katika kusaidia mazungumzo haya yaweze kufanyika, ili kama kuna uwezekano Halmashauri ya Mpanda iweze kunufaika pia, katika masuala hayo ambayo Mheshimiwa Mbunge ameyasema. Ahsante sana. (Makofi)