Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Energy and Minerals Wizara ya Madini 219 2025-05-05

Name

Sebastian Simon Kapufi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mpanda Mjini

Primary Question

MHE. SEBASTIAN S. KAPUFI aliuliza:-

Je, Halmashauri ya Mpanda inanufaika vipi na mauzo ya mchanga wa marudio ya madini katika Kata ya Misunkomilo, Mpanda? (Makofi)

Name

Anthony Peter Mavunde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dodoma mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI K.n.y. WAZIRI WA MADINI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kipindi cha kuanzia Julai, 2024 hadi Machi, 2025 jumla ya tani 2,498.16 za makinikia ya shaba (copper concentrates) zilichenjuliwa kutoka katika Kata ya Misunkomilo ambapo madini ya shaba yenye thamani ya shilingi bilioni 16.01 yalipatikana na Serikali kunufaika kwa kukusanya shilingi bilioni 1.12 kupitia mrabaha na ada ya ukaguzi. Aidha, jumla ya shilingi milioni 48.02 zilikusanywa, kama tozo ya huduma (service levy) ambapo, Halmashauri za Mpanda Mjini na Nsimbo zilinufaika. Ahsante.