Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Zahor Mohamed Haji
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mwera
Primary Question
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:- Je, Serikali imejiandaaje kukabiliana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Dawa za Kulevya kwani mbinu za uhalifu zimebadilika?
Supplementary Question 1
MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaishukuru Serikali kwa majibu mazuri, lakini ninaomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; mwaka 2023 Bunge lako lili-ratify Mkataba wa Kimataifa kwenye hoja ya kudhibiti biashara ya dawa ya kulevya pamoja na usafirishaji haramu wa binadamu. Je, sisi kama Serikali, tumeanza utekelezaji wake?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; kwa sababu, sasa ni mwaka wa pili, je, Serikali imeanza kufanya tathmini ili kuona faida, mafanikio na hasara ya ratification hii? Ahsante sana. (Makofi)
Name
Gibson Blasius Meiseyeki
Sex
Male
Party
CHADEMA
Constituent
Arumeru-Magharibi
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Zahor Mohammed Haji, Mbunge wa Mwera, kama ifuatavyo; ni kweli, mwaka 2023, kama nchi, tuliridhia Mkataba wa Kimataifa wa kupambana na usafirishaji haramu wa binadamu pamoja na dawa za kulevya. Utekelezaji huo tayari umeshaanza kufanya kazi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu swali la pili, tathmini imefanyika na ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba, tathmini ya kuridhia mkataba huu imekuwa na mafanikio makubwa sana na wanashuhudia jinsi hii biashara ya dawa za kulevya zinavyokamatwa mara kwa mara. Kwa hiyo, kwa kweli, tathmini imefanyika na mkataba huu umekuwa na manufaa makubwa sana hapa nchini. Ahsante sana.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved