Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 218 2025-05-05

Name

Zahor Mohamed Haji

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwera

Primary Question

MHE. ZAHOR MOHAMMED HAJI aliuliza:-

Je, Serikali imejiandaaje kukabiliana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu na Dawa za Kulevya kwani mbinu za uhalifu zimebadilika?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua uwepo wa uhalifu wa usafirishaji haramu wa binadamu hapa nchini na kwamba, mbinu za utendekaji wake zimekuwa zikibadilika. Katika kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu, Serikali ina mikakati mbalimbali, ikiwa ni pamoja na kuwa na Mpango Kazi wa Kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu, kutoa mafunzo kwa wasimamizi wa Sheria na wadau mbalimbali, kuratibu kampeni ya kutoa elimu kwa umma kuhusu uhalifu huu na madhara yake, mpango wa kuanzisha Kituo cha Kupokelea Taarifa za Usafirishaji Haramu wa Binadamu na mpango wa kuanzisha Mfumo wa Kielektroniki wa Kukusanya, Kusimamia na Kuhifadhi Taarifa za Usafirishaji Haramu wa Binadamu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukubaliana na mabadiliko ya mara kwa mara ya mbinu za uhalifu wa dawa za kulevya, Serikali imekuwa ikiwajengea uwezo maafisa wa udhibiti kwa kuwapatia mafunzo, ushiriki wa mikutano na vikao vya kimkakati vya kubadilishana taarifa za uzoefu na nchi na taasisi mbalimbali za kimataifa katika udhibiti wa dawa za kulevya. Ahsante. (Makofi)