Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Vituo vya Polisi, Kata za Kate na Kipande, kwani tayari maeneo yameandaliwa?

Supplementary Question 1

MHE. VINCENT P. MBOGO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Serikali imejenga Kituo Kipya cha Polisi, Kata ya Kala, Kijiji cha Mpasa. Askari wako pale hawana vitendea kazi na ukizingatia ni Ukanda wa Ziwa Tanganyika na Mheshimiwa Waziri aliahidi kupeleka boti pamoja na pikipiki kabla ya mwezi Machi, lakini mpaka sasahivi vifaa havijafika. Ni lini mnapeleka boti na pikipiki katika Kituo Kipya cha Polisi Mpasa? (Makofi)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vincent Paul Mbogo, Mbunge wa Nkasi Kusini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli, Serikali inatambua kwamba, kuna upungufu wa vitendea kazi kwenye Kituo cha Polisi alichokitaja. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan iko makini na imeongeza vitendea kazi vingi zikiwemo pikipiki pamoja na boti na ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tutapeleka vifaa hivyo, kwa ajili ya utendaji kazi katika eneo hilo. Ahsante sana. (Makofi)

Name

Ester Amos Bulaya

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Vituo vya Polisi, Kata za Kate na Kipande, kwani tayari maeneo yameandaliwa?

Supplementary Question 2

MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niulize swali dogo la nyongeza. Hali ya Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Bunda ambacho kinahudumia majimbo matatu; Bunda Mjini, Bunda kwa Getere pamoja na Mwibara ni mbaya. Ninataka kujua, ni lini watatujengea Kituo kipya cha Polisi chenye hadhi ya Wilaya ya Bunda na hasa ukuzingatia Mji wa Bunda unakua? Nimeliongelea sana hapa, kama Mbunge wa wananchi wa Jimbo la Bunda Mjini. (Makofi/Kicheko)

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikijenga Vituo vya Polisi vyenye hadhi vya mikoa, wilaya, kata pamoja na shehia hapa nchini. Wilaya ya Bunda pia ni wilaya ambayo ina majimbo matatu, kama alivyosema na tunatambua pia kwamba, wananchi hawa wanatakiwa kulindwa na mali zao. Ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, tumekichukua kituo hicho, tutakiweka kwenye mpango na kukitengea fedha kwa ajili ya kukijenga kwa hadhi ya Wilaya ya Bunda. Ahsante. (Makofi)

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:- Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Vituo vya Polisi, Kata za Kate na Kipande, kwani tayari maeneo yameandaliwa?

Supplementary Question 3

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Oliver Semuguruka.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Oliver Semuguruka.

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti...

MWENYEKITI: Sogea pembeni hapo.

MBUNGE FULANI: Njoo huku, za huku zinafanya kazi.

MWENYEKITI: Jaribu nyingine. Waheshimiwa, ninaomba utulivu tafadhali.

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru kwa kunipa nafasi..

MWENYEKITI: Kituo cha Polisi Wilaya ya Ngara, ninafikiri Mheshimiwa Waziri amesikia. Majibu Mheshimiwa.

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, bahati nzuri nilifika Ngara, ni kweli Kituo cha Ngara kipo kwenye hatua ya lenta. Ninampongeza sana Mheshimiwa Mbunge wa Mkoa pamoja na Mbunge wa Jimbo kwa ufuatiliaji na ninawapongeza wananchi kwa kutumia nguvu zao kujenga kituo hicho mpaka kufikia hatua ya lenta.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, Serikali imepanga kumalizia vituo 77 ambavyo ni maboma, kikiwepo pia, Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Ngara. Ahsante sana.

(Hapa vinasa sauti katika Ukumbi wa Bunge vilipata hitilafu)

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, ninaomba utulivu. Wanaohusika na mitambo, tafadhali ninaomba tuweke sawa, ili tuweze kusikilizana Bungeni. Tayari zinafanya kazi?

WABUNGE FULANI: Bado.

MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tuvumilie tu kidogo, watu wa IT wanashughulikia. Ni lazima tusikilizane Bungeni ili Hansard zetu ziweze kusoma vizuri.

Mheshimiwa Waziri, unaweza kukaa kwa dakika chache, ili tusubiri. Waheshimiwa Wabunge kwa busara tu, kuna upande wa pili huku zinafanya kazi. Mwenye swali anaweza kuja kuuliza huku; siyo upande huu, ni upande ule pale. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Waziri, sasa jaribu kujibu kwa upande huu. Mheshimiwa Waziri, basi jibu hapo, inafanya kazi. Endelea Mheshimiwa Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Oliver, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Kituo cha Polisi cha Ngara ni moja ya maboma 77 ambayo yametengewa fedha kwenye mwaka wa fedha 2025/2026, kwa ajili ya ukamilishaji. Ahsante sana.