Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 217 2025-05-05

Name

Vincent Paul Mbogo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nkasi Kusini

Primary Question

MHE. VINCENT P. MBOGO aliuliza:-

Je, lini Serikali itamaliza ujenzi wa Vituo vya Polisi, Kata za Kate na Kipande, kwani tayari maeneo yameandaliwa?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kate umefikia kwenye hatua ya umaliziaji na kiasi cha fedha, shilingi 25,000,000, kimetengwa kwenye Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2024/2025. Katika Kata ya Kipande limetengwa eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 8,092 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi cha Kata, utakaogharimu shilingi 115,000,000. Fedha hizo zitatengwa kwenye mwaka wa fedha 2026/2027. Ahsante. (Makofi)