Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:- Je, kuna mpango gani wa kusitisha kutoa vibali kwa mashine za Kamari ili kupunguza umaskini kwa Vijana?

Supplementary Question 1

MHE. MUHARAMI S. MKENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, nina swali moja la nyongeza. Mashine hizi za slot zimemwagika nyingi sana mtaani, lakini majibu yake aliyoyatoa ni mazuri sana. Kuna hili suala la betting ambalo kuna vibanda vingi sana vimefunguliwa katika miji yetu na maeneo mbalimbali. Vijana wetu wanafanya betting na kujitia umaskini katika kufanya jambo hili. Je, Serikali ina mpango gani sasa wa kuzuia hizi betting, ili vijana wetu waende vizuri katika uchumi wao? Ninashukuru. (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Muharani Mkenge, lakini kabla ya kujibu ninampongeza sana kwa namna anavyofuatilia suala hili, ili kulinda maadili ya vijana wetu na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninaomba niielekeze Bodi ya Michezo ya Kubahatisha kuendelea na zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara na ufuatiliaji wa karibu sana ili kuhakikisha Sheria na taratibu zimefuatwa, ili kuhami na kunusuru vijana wetu katika suala zima la maadili. Ahsante sana.