Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Finance Wizara ya Fedha 216 2025-05-05

Name

Muharami Shabani Mkenge

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bagamoyo

Primary Question

MHE. MUHARAMI S. MKENGE aliuliza:-

Je, kuna mpango gani wa kusitisha kutoa vibali kwa mashine za Kamari ili kupunguza umaskini kwa Vijana?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la waendeshaji mashine za slots pasipo kuzingatia sheria za michezo ya kubahatisha na sheria nyingine za nchi. Mathalani, waendeshaji haramu huweka mashine zao kwenye makazi ya watu, maduka ya bidhaa, maeneo ya vijijini na pia huruhusu watu wa chini ya miaka 18 kushiriki katika michezo hiyo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na changamoto hizi, bodi imechukua hatua kadhaa kama ifuatavyo: -

(i) Kusitisha utoaji wa leseni kwa waendeshaji wapya wa mashine za sloti;

(ii) Kuanzisha misako na operation ya kusaka waendeshaji haramu wa mashine za sloti nchi nzima kwa kushirikiana na mamlaka nyingine kama vile Polisi, TRA na Uhamiaji;

(iii) Kuongeza kaguzi za mara kwa mara katika maeneo mbalimbali ya nchi ilipo biashara ya mashine za sloti;

(iv) Kuendesha kampeni inayowalenga vijana na jamii kufanya kazi za uzalishaji;

(v) Kuongeza udhibiti wa uingizaji wa mashine za sloti hapa nchini kwenye maeneo ya mipakani kwa kushirikiana na TRA;

(vi) Kuanza mchakato wa kutumia mifumo ya kielektroniki kudhibiti biashara ya mashine za sloti zinazoendeshwa mitaani;

(vii) Kuingia makubaliano (MoU) na Mamlaka ya Serikali za Mitaa kwa lengo la kuwa na ushirikiano wa karibu wa kudhibiti waendeshaji haramu wa mashine za sloti; na

(viii) Kupitia mara kwa mara Sheria ya Michezo ya Kubahatisha kwa lengo la kuondoa kasoro na mianya inayotumiwa na waendeshaji haramu wa mashine za sloti.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Bodi inakusudia kutekeleza hatua hizi kikamilifu ikiwa ni sehemu ya juhudi yake ya kuhakikisha kuwa, jamii ikiwemo vijana inalindwa dhidi ya athari hasi za michezo ya kubahatisha ikiwemo umaskini. Bodi itaendelea kuchukua hatua zaidi za kuondoa athari zote hasi za michezo ya kubahatisha. Ahsante sana.