Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mariamu Nassoro Kisangi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y MHE. SAADA MANSOUR HUSSEIN aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha matumizi ya mkaa mbadala yanaenezwa hadi Zanzibar?

Supplementary Question 1

MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba, maeneo yote katika nchi ya Tanzania wanapata nishati hiyo mbadala?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante, ninashukuru kwa swali la nyongeza la Mheshimiwa Mariam Kisangi, ni kweli Serikali inao mkakati kupitia STAMICO, miezi michache iliyopita makontena haya yalisambazwa kwenye mikoa mbalimbali kulingana na zone zake, kwenye ile mikoa ambayo haijafikiwa pia STAMICO wanao mkakati wa kuendelea kupeleka makontena haya ili kuhakikisha mkaa huu wa Rafiki Briquettes unaendelea kutumika katika maeneo yote ya nchi. Kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, Serikali inao mkakati sasa hivi makontena yamefika kwenye mikoa mingi na tutaendelea hivyo hivyo kwa awamu zinazokuja.