Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Energy and Minerals Wizara ya Nishati 215 2025-05-05

Name

Saada Mansour Hussein

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARIAM N. KISANGI K.n.y MHE. SAADA MANSOUR HUSSEIN aliuliza:-
Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha matumizi ya mkaa mbadala yanaenezwa hadi Zanzibar?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuhakikisha kwamba, matumizi ya mkaa mbadala yanaenezwa hadi Zanzibar, Serikali kupitia Shirika la Madini (STAMICO) imesajili mawakala wanne kwa ajili ya kuhakikisha mkaa mbadala uitwao Rafiki Briquettes unafika Zanzbar.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mawakala hawa ni Chama cha Ushirika, Maisha Gemu, Salum Omar, Easy Fix na Wanawake na Samia Magharibi B. Aidha, juhudi pia zinafanyika ili kupata eneo ambalo STAMICO wataweka kontena kubwa ambalo litakuwa linapokea mkaa huu mbadala wa Rafiki Briquettes ili kuihifadhi kwa ajili ya kusambazwa katika maeneo yote ya Zanzibar.