Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, upi mpango wa Taifa wa kupanda miti kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu ili kukabiliana na janga la kukata miti?
Supplementary Question 1
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali ya nyongeza. Swali la kwanza; majangili wanaotumia msumeno nyororo au chainsaw, wamekuwa kikwazo kikubwa sana kwa Serikali kwa sababu wanaharibu mazingira ya miti iliyopadwa, miti ya asili na ile ambayo inatunza vyanzo vya maji. Je, Serikali inatoa tamko gani kuhusu ujangili huu?
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; je, mnayo mipango gani ya kufuatilia na kufanya tathmini ya miradi ambayo umeitaja ya kupanda miti ili kuangalia kama ufanisi au changamoto katika miradi ambayo inatekelezwa hapa nchini? (Makofi)
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU K.n.y WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa maswali mawili ya Mheshimiwa Profesa Ndakidemi, moja hili la kuhusiana na matumizi ya chain saw.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, pamoja na kuwa mashine hizo zipo zinauzwa hapa nchini, lakini kuna utaratibu maalum ambao upo kwa mujibu wa mwongozo kwamba zisitumike hovyo kwenye maeneo ambayo hayajapewa kibali, matumizi yoyote ya chain saw siyo tu kwa Kilimanjaro, lakini nitoe maelekezo kwa nchi nzima kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira kwamba ni marufuku kwa mtu yeyote kutumia mashine ya chainsaw bila kuwa na kibali halali kutoka kwenye mamlaka zilizopo kwenye maeneo hayo na hasa Halmashauri.
Mheshimiwa Mwenyekiti, pili, kwenye maeneo hata yale ya misitu ambayo ipo kwa mujibu wa sheria na inatambulika kwenye maeneo mbalimbali kwa mujibu wa maeneo na Halmashauri au Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, huko nako pia kuna utaratibu wake wa kuweza kutumia, hata kule kuliko na miti ambayo imepadwa namna ya uvunaji kuna utaratibu maalum.
Mheshimiwa Mwenyekiti, ninatoa maelekezo kwamba, ni muhimu wazingatie utaratibu wa kikanuni na kisheria uliowekwa katika matumizi ya chain saw, kama atakiuka mtu tutachukua hatua kali sana za kisheria kupitia zetu za Mikoa na Wilaya.
Mheshimiwa Mwenyekiti, swali lake la pili, ni kwamba, zipo timu kuhusiana na suala la monitoring and evaluation ambazo zinafanya monitoring and evaluation mojawapo ni maafisa viungo walio katika maeneo yote huku nchini hasa kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa ambao wanafanya kazi hii ya kuhakikisha kwamba upandaji miti unafanyika, lakini hata ile ambayo imeharibiwa basi waweze kuchukua hatua. Wapo vile vile Maafisa Mazingira kwenye Halmashauri zetu zote na wanalipwa na Serikali hii ni waajiriwa.
Mheshimiwa Mwenyekiti, wapo pia mabalozi wa mazingira na hivyo hivyo wapo mameneja wa NEMC katika mamlaka zote za Mikoa na Wilaya ambao wanasimamia suala hili, ikiwa ni sambamba na TARURA ambao wapo chini ya Ofisi ya TAMISEMI nao wanafanya kazi ya kuhakikisha kwamba miti yote iliyopandwa pembezoni mwa barabara inaendelea kustawi pia kukaa katika hali ambayo inaweza ikaleta usaidizi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kubwa zaidi ni kwamba, Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Wakurugenzi na Mamlaka zote za Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa wanalo agizo mahususi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na wanafahamu kwamba maagizo haya yalikuwa ya Mheshimiwa Rais mwenyewe ambaye ni champion wa mazingira ndiyo maana akaanzisha program mbalimbali za kuweza kuhakikisha kunakuwa na ustawi. Ahsante. (Makofi)
Name
Khalifa Mohammed Issa
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Mtambwe
Primary Question
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:- Je, upi mpango wa Taifa wa kupanda miti kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu ili kukabiliana na janga la kukata miti?
Supplementary Question 2
MHE. KHALIFA MOHAMED ISSA: Mheshimiwa Mwenyekiti, Kuna wimbi kubwa la ukataji wa miti ya mikoko katika ukanda wa bahari hasa Zanzibar na kusababisha maji ya bahari kupanda, kuvamia katika makazi ya watu. Je, Serikali ina mpango gani wa kuweza kusimamia program ya upandaji wa miti ya mikoko na kuweza kuilinda ili kuepuka athari za tabianchi? Ahsante sana.
Name
Paschal Katambi Patrobas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Shinyanga Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU K.n.y WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA: Mheshimiwa Mwenyekiti, suala hili ndiyo maana unaona lipo chini ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira. Mipango ambayo ipo chini ya ofisi hii ambayo inasimamiwa na Makamu wa Rais lakini pia Waziri wa Nchi, Mheshimiwa Masauni pamoja na Naibu Waziri Chilo na Katibu Mkuu Luhemeja, wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kukutana na pande zote mbili za Muungano ili kuweza kuweka mikakati madhubuti ya kudhibiti uharibifu wa mazingira.
Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo hiki nilichokisema kwenye jibu langu la awali kipo pia katika upande wa Zanzibar na Mheshimiwa Dkt. Hussein Mwinyi anafanya kazi nzuri sana wakishirikiana na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha mambo yanakwenda sawasawa katika mazingira kwa sababu tukitambua uhai wetu unategemea sana mazingira mazuri. Ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved