Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 17 Union Affairs Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano 214 2025-05-05

Name

Prof. Patrick Alois Ndakidemi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Moshi Vijijini

Primary Question

MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI aliuliza:-

Je, upi mpango wa Taifa wa kupanda miti kwa kipindi cha muda mfupi na mrefu ili kukabiliana na janga la kukata miti?

Name

Eng. Hamad Yussuf Masauni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kikwajuni

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU K.n.y WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Profesa Patrick Aloyce Ndakidemi, Mbunge wa Moshi Vijijini kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI na Wizara ya Maliasili na Utalii, inatekeleza mpango wa muda mrefu na muda wa kati kuweka mikakati wa kurejesha na kupanda miti maeneo yaliyoharibiwa takribani hekta millioni 5.2 ifikapo 2030. Shughuli zinazoendelea ni pamoja na kuhamasisha wananchi kutunza mazingira kupitia kampeni za upandaji miti milioni 1.5 kwa kila Halmashauri kwa kila mwaka na Kampeni maalum ya ‘Soma na Mti’ ambapo Serikali itahakikisha wanafunzi wote wa shule za msingi, sekondari na vyuo vikuu kupanda miti na kuitunza katika kipindi chao chote cha masomo wawapo mashuleni na vyuoni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali kupitia Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) imeendelea kuzalisha miche ya miti ya aina mbalimbali na kuigawa bure kwa Wizara na Taasisi, Wadau, Sekta Binafsi pamoja na wananchi kwa lengo la kupanda miti katika maeneo yao kwa ajili ya kuhakikisha kwamba wanarejesha uoto wa asili nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kupitia Bunge lako Tukufu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania naomba kutoa rai kwa wananchi na sekta binafsi kuendelea kupanda miti kwenye maeneo mbalimbali nchini ili kukabiliana na uharibifu wa ardhi na kuenea kwa jangwa na ukame.