Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:- Je, lini Serikali italipa madeni ya Walimu wa Shule za Sekondari waliohamishiwa Shule za Msingi?

Supplementary Question 1

MHE. SAASISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza ninawapongeza Walimu wote wa Shule za Msingi na Shule za Sekondari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kutoa elimu kwa wanafunzi wetu katika Wilaya ya Hai. (Makofi)

Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya pongezi hizo nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza; katika Wilaya ya Hai kuna Walimu 184 ambao walihamishwa kutoka shule za sekondari kwenda shule za msingi, wanaidai Serikali sasa hivi milioni 120. Je, ni lini Serikali italipa madeni haya ya watumishi ambao wamehama kutoka Shule ya Msingi kwenda Sekondari?

Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la pili; Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI alikutana na watumishi wastaafu katika Wilaya ya Hai na watumishi ambao siyo walimu, nao wanadai shilingi milioni 915 na tayari Waziri alikusanya taarifa zao, lakini mpaka sasa hivi watumishi hao wastaafu na walioko kazini ambao siyo walimu hawajalipwa fedha zao. Je, ni lini Serikali italipa madeni kwa watumishi hawa ambayo yamekuwa ni kero kwao?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua kazi kubwa sana na nzuri inayofanywa na watumishi wetu ikiwemo watumishi katika kada ya elimu. Serikali imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali kuhakikisha kwamba inaendelea kuboresha maslahi ya watumishi hawa muhimu, mojawapo ni kuhakikisha kwamba inaendelea kuchukua jitihada za kuwalipa stahiki zao; na Mheshimiwa Mbunge tayari alinifuata akanielezea madai ya watumishi hawa kutoka katika Jimbo lake na ninachoomba kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge ni kwamba, jambo hili kwa sababu ulishalileta tunalifanyia kazi ili liweze kupata Suluhu, watumishi wetu hawa tunatambua kazi kubwa wanayoifanya na tunatambua kwamba wana kila haki ya kuweza kupata stahili zao na tutasimamia ili tuweze kutekeleza kwa wakati jambo hili la kuwalipa stahili zako.