Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Finance and Planning Wizara ya Viwanda , Biashara na Uwekezaji 213 2025-05-05

Name

Saashisha Elinikyo Mafuwe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Hai

Primary Question

MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza:-

Je, lini Serikali italipa madeni ya Walimu wa Shule za Sekondari waliohamishiwa Shule za Msingi?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika kuboresha ikama ya walimu wa shule za msingi nchini imekuwa ikihamisha walimu kwa kuzingatia ikama ya Halmashauri husika.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kipindi cha mwaka 2017 hadi 2025, walimu 1,914 wamehamishwa kutoka shule za sekondari kwenda shule za msingi. Fedha iliyohitajika kwa ajili ya uhamisho huo ni shilingi bilioni 2.08 ambapo shilingi bilioni 1.22 zimelipwa na kiasi ambacho hakijalipwa ni shilingi milioni 865.93. Serikali itaendelea kulipa madeni ya uhamisho wa walimu kadri ya upatikaji wa fedha.